NAFASI 60 KAZI ZA AFISA MRADI WA MALIPO YA KABONI
NAFASI 60 KAZI ZA AFISA MRADI WA MALIPO YA KABONI
- Kusimamia uandikishaji wa wakulima waliokidhi vigezo vya mradi.
- Kutoa mafunzo na kufuatilia maendeleo ya upanzi, utunzaji na maendeleo ya miti na mazao
- Kukusanya na kufuatilia taarifa za mashambani kwa kushirikiana na wakulima.
- Kutoa mrejesho wa maendeleo na changamoto kwa msimamizi wa Malipo ya Kaboni.
- Kushirikiana na wakulima katika kufanikisha utekelezaji wa mafanikio ya mradi
- Awe na elimu ya astashahada (Certificate) katika kilimo, mazingira, maendeleo ya jamii au maeneo yanayohusiana.
- Awe na uwezo mzuri wa kuwasiliana kwa Kiswahili fasaha.
- Awe na ujuzi katika masuala ya teknolojia na ukusanyaji wa data.
- Awe na uzoefu wa kufanya kazi na wakulima, hasa katika maeneo ya vijijini.
- Awe na uwezo wa kufanya kazi katika mazingira ya kijijini na kusafiri umbali mrefu.
- Awe na viambatanisho mhimu vifuatavyo Nakala ya kitambulisho au namba ya NIDA, Nakala ya cheti cha kuzaliwa au kitambulisho cha mpiga kura Nakala za vyeti vya elimu (kuanzia kidato cha nne, astashahada n.k,)
- Hakikisha maombi yako yanaonyesha mahali ulipo kwa sasa, wilaya unayoomba kufanyia kazi, Vijiji angalau 3 unavyopendelea kufanya kazi, na Ueleze kama uko tayari kufanya kazi katika vijiji vingine tofauti na ulivyo pendekeza. Tazama hapa Orodha ya Vijiji vyenye nafasi za Kazi.
- Wasilisha maombi (barua yako ya maombi na wasifu (CV) kwenye ofisi zetu au maduka ya OAF yaliyopo mikoa ya Iringa na Njombe.
- Kwa Njia ya Mtandaoni (Online), Tuma barua yako ya maombi na wasifu (CV) kwa njia ya mtandao kupitia tovuti hii ya mtandao https://forms.gle/mSf8KmbQcqnaTQPL7
- Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya kazi ni: 15 September, 2024
