NAFASI 40 za Wakusanya Mapato Geita District Council
NAFASI 40 za Wakusanya Mapato Geita District Council
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Geita anapenda kuwatangazia Wananchi wote wenye sifa, nafasi Arobaini (40) za Ajira ya Mkataba ya wakusanya Mapato katika Halmashauri ya Wilaya Geita.
Sifa za Mwombaji
- Mwombaji awe Raia wa Tanzania.
- Awe amehitimu Kidato cha Nne na kuendelea.
- Awe na Mdhamini mwenye mali isiyo hamishika.
- Awe Mwadilifu na ambaye hajawahi kukutwa na hatia Mahakamani.
- Awe na uwezo wa kufanya kazi kwa kujituma bila kusimamiwa.
- Awe tayari kufanya Kazi katika Kata yoyote kwa kipindi kisichopungua Mwaka Mmoja.
- Awe na Umri wa kuanzia Miaka 18 hadi 45.
Kazi na Majukumu
- Kukusanya Mapato ya Halmashauri ya Wilaya Geita
Mambo ya Jumla ya Kuzingatia.
- Nakala ya Cheti cha Kidato cha Nne na kuendelea.
- Waombaji waambatishe Vivuli vya Vyeti vya Elimu vilivyothibitishwa na Wakili, maelezo binafsi (CV),
- Nakala ya Cheti cha kuzaliwa.
Katika barua ya maombi, weka Namba yako ya simu inayopatikana muda wote. - Barua zibandikwe picha mbili (2) – Passport size.
- Waombaji watakaokidhi sifa na vigezo watajulishwa tarehe ya usaili.
- Maombi yote yaambatane na barua za Wadhamini Wawili zinazoonesha Mali zisizohamishika.
Maombi yote yaelekezwe Ofisi ya Mkurugenzi Wilaya ya Geita kwa Anuani ifuatayo:-
Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashauri ya Wilaya ya Geita,
S.L.P 139,
GEITA
Mwisho wa kupokea maombi ni 16/12/2024 saa 9:30 alasiri
