NAFASI 35 za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro November 2024
NAFASI 35 za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro November 2024
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, inatangaza nafasi 35 za kujitolea kwa Kada mbalimbali kwa muda wa miezi kumi na mbili (12) kama ifuatavyo:-
✅Afisa Muuguzi Msaidizi Nafasi – 18.
✅Afisa Tehama Nafasi – 1.
✅Mapokezi Nafasi – 4.
✅Wapaguzi Nafasi – 4.
✅Wahudumu wa chumba cha Maiti Nafasi – 2.
✅Mpiga Picha Nafasi – 1.
✅Radiographer Nafasi – 5.
Jumla Nafasi – 35.
SIFA ZA JUMLA KWA KADA ZA AFYA:
Waombaji wanatakiwa kuwa na:-
- Cheti cha taaluma cha kada aliyosomea cha chuo. kinachotambuliwa na Serikali
- Awe amesajiliwa na Baraza la Kitaaluma kwa Kada za Afya.
- Awe na Leseni ya taaluma husik.a
- Awe na cheti cha kidato cha nne/sita kinachotambuliwa na NECTA.
SIFA ZA JUMLA KWA KADA ZISIZO ZA AFYA
Waombaji wanatakiwa kuwa na:-
- Cheti cha taaluma cha kozi aliyosomea cha chuo kinachotambuliwa na Serikali
- Awe anajua Kiswahili na Kingereza
MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI
Waombaji wote wanatakiwa kuwa na sifa za jumla kama ifuatavyo:-
- Awe raia wa Tanzania.
- Awe na umri usiozidi miaka 45.
Awe na vyeti kamili vya mafunzo ya fani aliyosomea (Cheti cha Kidato cha Nne, Sita, Taaluma na Usajili kamili) “Full Registration” au Leseni hai ya kufanya kazi ya taaluma husika.
- Mwombaji awe hajawahi kupatikana na kosa la jinai au kufungwa jela.
- Maombi yaambatane na wasifu wa waombaji.
Maombi yaambatanishwe na nakala za vyeti vya Elimu, Taaluma na Cheti cha kuzaliwa Testimonals results slip HAITAKUBALIWA
Maombi yatumwe kwa:-
Mganga Mfawidhi,
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro
S.L.P.110
MOROGORO
Mwisho wakupokea maombi ni taehe 20/11/2024

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Tags: NAFASI 35 za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro November 2024