NAFASI 332 za Kazi Shirika la Afya MDH Tanzania
NAFASI 332 za Kazi Shirika la Afya MDH Tanzania
Management and Development for Health (MDH) ni shirika lisilo la kiserikali ambalo lengo lake kuu ni kuchangia na kushughulikia vipaumbele vya huduma za Afya kwa umma kwaajili ya ustawi wa jamii.
Vipaumbele hivi ni pamoja na kuzuia kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza kama vile VVU/UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria, kutekeleza huduma za Afya ya uzazi kwa wakina mama, vijana na watoto wachanga, na kusimamia afua za lishe. Pia kutoa huduma za kuzuia magonjwa yasio ya kuambukiza kama vile saratani ya mlango wa kizazi, shinikizo la juu la damu na elimu kuhusu mtindo bora wa maisha, pamoja na uimarishaji wa mifumo ya Afya.
MDH inaamini na inafanya kazi kwa ushirikiano wa wadau wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi, Wizara ya Afya, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wenye Ulemavu, Wazee na Watoto,
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), mashirika ya wafadhili mbalimbali, taasisi za kitaaluma na zisiszo za kitaaluma, washirika wa utekelezaji, asasi za kiraia,
mashirika ya kijamii, kidini na taasisi nyinginezo.
MDH kwa kushirikiana na Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam na Hospitali za Rufaa inawakaribisha wananchi wenye vigezo kuomba nafasi zifuatazo za kazi za kujitolea:
Nafasi za kazi zilizotangazwa ni kama ifuatavyo hapa chini;
✅Mteja Mtaalamu Idara ya Magonjwa ya Nje (OPD Expert Client) Halmashauri za:
- Jiji la Dar es Salaam nafasi – 44.
- Temeke MC nafasi – 46.
- Kinondoni MC nafasi – 30.
- Kigamboni MC nafasi – 22.
- Ubungo MC nafasi – 24.
Msimamizi: Msimamizi wa kituo (Site Supervisor)
Muhtasari wa Kazi:
Mteja mtaalam anatakiwa kutoa elimu ya Afya kuhusu upimaji wa V.V.U na huduma kinga dhidi ya maambukizi mapya ya V.V.U,Kufanya uchunguzi wa kutambua watu wenye sifa ya kupatiwa
huduma za upimaji wa V.V.U na kuwaungaisha na huduma za Upimaji wa V.V.U
Majukumu ya Kazi:
Mteja mtaalam/mzoefu atapaswa kutoa ushauri nasaha juu ya maambukizi ya VVU kulingana na muongozo wa Wizara ya Afya na kwa kushirikiana na watoa huduma katika ngazi ya hospitali/
kituo cha afya/zahanati:
- Kuhamasisha uchunguzi wa sifa za upimaji wa VVU wenye tija (optimized providerinitiated testing and counseling – (oPITC) modal na huduma kinga dhidi ya maambukizi ya V.V.U
- Kutoa huduma ya uunganishwaji na ufuatiliaji kulingana na muongozo wa extended linkage case management (eLCM) modal.
- Kuhakikisha zaidi ya asilimia 95 (>95%) ya wagonjwa na wasindikizaji wao wasio fahamu hali zao za maambukizi wanaofika kituoni wanapatiwa huduma ya uchunguzi wa awali kwa ajili ya kutambua hali zao za maambukizi ya VVU
- Kuhakikisha wateja wote (100%) wenye sifa za upimaji wanapatiwa huduma ya upimmaji ili kutambua hali zao za maambukizi
- Kutoa ushauri nasaha kabla na baada ya kupima maambukizi ya VVU
- Kushirikiana na kiongozi wa upimaji kituoni kuhakikisha wateja wote wenye majibu chanya wanaunganishwa katika huduma ya ufuatiliaji (eLCM)
- Kusaidia wateja wapya kujua sehemu mbalimbali za utoaji wa huduma mfano kipimo cha CD4 na sehemu ya kuchukulia dawa za ARV au Dawa Kinga.
- Kuhakikisha ujazaji sahihi na timilifu wa vitabu na fomu zote za huduma ya upimaji na ungwanishwaji. (HIV Screening register and eLCM Master form)
- Kuhakikisha ufuatiliaji sahihi wa mteja kulingana na mfumo wa huduma za upimaji na uunganishwaji.
- Kuhakikisha uandikishaji na utunzaji wa nyaraka zote za huduma ya upimaji na uunganishwaji
- Kutekeleza majukumu mengineyo kama atakavyoelekezwa na msimamizi wake wa kazi
Vigezo: Elimu, uzoefu wa kazi na ustadi
Awe na sifa zifuatazo:
- Amehitimu elimu ya shule ya msingi na anaweza kusoma, kuhesabu na kuandika
- Anayeweza kujiweka wazi juu ya Hali yake ya Kuishi na V.V.U
- Awe ni mfuasi mzuri wa dawa za kufubaza V.V.U
- Umri usiozidi miaka Arobaini na tano (45)
- Anaishi kwenye kata/kijiji kilichopo kituo anachoomba kujitolea
- Uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha kwa lugha ya Kiswahili
- Uwezo wa kutunza siri katika nyanja zote
- Uthibitisho wa kuwa mteja mzoefu
✅Muelimishaji rika ngazi ya Jamii
Halmashauri za:
- Jiji la Dar es Salaam nafasi – 45.
- Kinondoni MC nafasi – 41.
- Ubungo MC nafasi – 31.
- Temeke nafasi – 39.
- Kigamboni nafasi – 10.
Msimamizi: Msimamizi wa kituo (Site Supervisor)
Muhtasari wa kazi:
Muelimisha rika ngazi ya jamii anajukumu la kutambua,kuandaa vijiwe na kutoa elimu/hamasa juu ya huduma za upimaji wa V.V.U na huduma kinga dhidi ya maambukizi ya V.V.U kwa watu
wote na ambao wako kwenye hatari zaidi ya kuambukizwa V.V.U
Majukumu ya Kazi
- Utambuzi wa vijiwe/maeneo ya kutolea huduma kuomba ridhaa ya kutoa huduma kwa wamiliki mbalimbali kwenye Jamii.
- Kutoa elimu kwa wateja wa makundi maalumu na yaliyopewa kipaumbele kwenye jamii
kuhusu kubadili tabia hatarishi, huduma ya dawa kinga na upimaji wa VVU. - Kusaidia ufuasi mzuri wa dawa na ratiba za mahudhurio ya kliniki kwa wateja wa dawa kinga (PrEP).
- Kuchukua na kutunza kumbukumbu, kuripoti na ufuatiliaji wa kila siku, kila wiki, kila mwezi na robo mwaka.
- Kuimarisha ufuasi sahihi wa dawa kwa kushirikiana na watumishi wa Afya katika kuwafuatilia wagonjwa/wateja wanaoshindwa kuhudhuria kliniki kwa tarehe
walizopangiwa. - Kuwa mfano bora kwa kutumia uzoefu wao kama watu wa makundi maalumu kwa kuwashauri wenzao kuishi kwa matumaini na kuwapa mbinu za kujikinga na maambukizi mapya ya VVU.
- Kushirikiana na wapimaji wa VVU kuandaa ripoti ya kila siku, wiki na mwezi.
- Kusaidia wagonjwa wapya kufahamu maeneo muhimu kituoni na kuboresha ufanisi wa rufaa baina ya vitengo mbalimbali kituoni mfano kutoka kliniki ya wagonjwa wa nje (OPD) kwenda kliniki ya tiba na matunzo (CTC), kliniki ya Afya ya uzazi na watoto (RCH) n.k.
- Kusaidia kuwaunganisha wateja wa makundi maalumu na huduma mbalimbali zilizopo katika vituo vya afya/jamii, hususani huduma za dawa kinga, ARVs, Uzazi wa mpango n.k.
- Kufanya majukumu mengine atakayopangiwa na msimazi wake.
Vigezo: Elimu, uzoefu wa kazi na ustadi
Awe na sifa zifuatazo
- Amehitimu elimu ya shule ya msingi na anaweza kusoma, kuhesabu na kuandika.
- Uzoefu wa mwaka mmoja (1) wa kufanya kazi ya uelimishaji rika ngazi ya jamii kwenye maswala ya VVU.
- Umri usiozidi miaka thelathini na tano (35)
- Anaishi kwenye kata/kijiji anachoomba kujitolea.
- Uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha kwa lugha ya Kiswahili.
- Uwezo wa kutunza siri katika nyanja zote.
- Utayari wa kufanya kazi nje ya masaa ya kawaida ya kazi.
Jinsi ya kutuma maombi ya nafasi za kazi:
Mwombaji katika nafasi yoyote kati ya zilizoainishwa hapo juu atatakiwa kuwasilisha viambatanishi vifuatavyo:
- Barua yao ya maombi ya kazi
- Wasifu wake (Resume/Curricula Vitae – CV)
- Barua ya utambulisho kutoka kwa mtendaji/mwenyekiti wa kata/kijiji anachotokea
- Nakala za vyeti vya elimu.
- Uthibitisho wa kuwa mteja mzoefu
- Nakala ya kitambuisho cha Taifa (NIDA) au kadi ya mpiga kura
Maombi yawasilishwe katika ofisi za halmashauri husika kabla ya tarehe 15 Novemba, 2024.
Tahadhari: MDH haina mawakala wowote na haitozi ada (gharama) yoyote kwa waombaji wa kazi hizi.
