NAFASI 3000 za Kazi Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi La Polisi (TPFCS)
NAFASI 3000 za Kazi Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi La Polisi (TPFCS)
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali La Jeshi La Polisi (TPFCS) kupitia kampuni ya Shirika ya Ulinzi (URA SECURITY) anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na Uwezo wa kujaza nafasi kama ifuatavyo;
✅ULINZI (Nafasi 3000)
SIFA ZA MUOMBAJI
- Awe Mtanzania mwenye umri kati ya 18-55
- Awe na Elimu kwanzia darasa la saba na kuendelea.
- Awe ni raia wa Tanzania kwa uthibitisho wa cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha taifa au hati ya kusafiria
• Awe na uwezo wa kusoma, kuandika na kuongea kwa ufasaha lugha ya kiswahili. - Asiwe na tuhuma yoyote Mahakamani au kuwahi kuhukumiwa kwa kosa la jinai
- Awe tayari kufanya kazi sehemu yoyote atakayopangiwa
Awe na afya njema (utimamu wa mwili) - Asiwe na michoro (tattoo) yoyote katika mwili wake
MAJUKUMU YA KAZI ZA WALINZI (SECURITY GUARDS)
- Kuhakikisha usalama wa watu na mali zilizopo eneo la kazi
- Kuzuia vitendo vya uhalifu sehemu ya kazi
- Kuzuia wizi na majanga ya moto eneo la kazi
- Kufanya doria eneo atakalopangiwa
- Kusimamia eneo la kupaki magari lililopo eneo la kazi
- Kutoa huduma nzuri kwa mteja eneo la kazi
- Pamoja na majukumu mengine atakayopangiwa na uongozi
VITU VINAVYOHITAJIKA KWENYE MAOMBI YA KAZI
Muombaji awe na:
- Barua ya Mkono ya Muombaji kazi.
- Barua ya utambulisho kutoka serikali za Mitaa
- Kivuli cha Kitambulisho cha Taifa au Namba ya utambulisho (NIN) (NIDA/MPIGA KURA)
- Vivuli vya Vyeti vya mafunzo ya JKT/JKU/MG, na passport size moja iliyopigwa hivi karibuni,
- Wasifu wa Muombaji (CV) na namba ya Simu
- Hati ya Tabia Njema (Finger Print).
- Wadhamini wawili watumishi wa Serikali / taasisi inayotambuliwa kisheria.
Wadhamini wawe na:
- Barua ya Mkono ya Udhamini.
- Barua ya Utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa na Passport Size 1.
- Kivuli cha kitambulisho cha Taifa/NIN (NIDA/MPIGA KURA).
- Kivuli cha kitambulisho cha Kazi
MASHARTI YA AJIRA
Ajira hii ni ya Mkataba.(renewable)
UTARATIBU WA UOMBAJI
NB: Maombi yanaweza kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili au Kingereza na kutumwa/ kuwasilishwa Ofisini kwa anwani ifuatayo:-
MKURUGENZI MTENDAJI,
SHIRIKA LA UZALISHAJI MALI LA JESHI LA POLISI,
S.L.P 79429,
DAR ES SALAAM.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15 Novemba 2024 saa 9:30 alasiri na wale watakaokuwa wamekidhi vigezo wataitwa kwenye usaili.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Tags: NAFASI 3000 za Kazi Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi La Polisi (TPFCS)