NAFASI 30 Za Kazi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Njombe

NAFASI 30 Za Kazi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Njombe
NAFASI 30 Za Kazi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Njombe
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Njombe kwa kushirikiana na shirika la USAID Afya Yangu (My Health) Southern Project imekuwa ikitekeleza Afua za kupambana na VVU/UKIMWI na Kifua kikuu katika Halmashauri zote za Mkoa wa Njombe.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe inakaribisha maombi ya kazi ya Muda (Miezi kumi) kutoka kwa watanzania wenye sifa, uwezo na ujuzi wa taaluma za Afya.
Watumishi watapangiwa kufanya kazi katika Vituo vya Kutolea Huduma za Afya vilivyopo katika Halmashauri za Mkoa wa Njombe.
Nafasi zinazotangazwa ni kama ifuatavyo:-
✅WAPIMAJI VVU WA HIYARI – NAFASI 30 (Njombe Mji 7, Mji Wa Makambako 1, Njombe Vijijini 8, Makete 3, Ludewa 5, Wanging’ombe 6)
MAJUKUMU YA KAZI.
- Uhamasishaji na elimu juu ya uwepo wa Huduma za Kupima VVU (HTS) yaani kuelimisha wateja juu ya masuala yote ya magonjwa ya VVU na usimamizi wa matibabu pamoja na maisha ya kimsingi ya afya.
- Kufanya upimaji wa VVU kwa washirika wa ngono wa mpokea huduma kwa kufuata kanuni 5 za upimaji wa VVU (usiri, ushauri nasaha, ridhaa, majibu sahihi na kuunganisha na huduma za matunzo na tiba).
- Kuwafikia washirika wa ngono halisi wa wapokea huduma, wenza wanaotumia pamoja vifaa vya kujidunga, wazazi wa kibaiolojia wa mpokea huduma mtoto, kwa ajili ya kuwapa huduma za upimaji wa VVU.
- Kufanya kwa ukamilifu uunganishaji na rufaa kwenye huduma za kuzuia maambukizi ya VVU kama ugawaji wa mipira ya kiume, vifaa vya kujipima mwenyewe VVU, huduma za kuzuia maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto na huduma za tohara ya hiyari kwa wanaume.
- Kuhakikisha vipimo vya uhakiki ubora na udhibiti ubora (QA/ QC) wa vifaa vya majaribio kwa nyenzo/sampuli za udhibiti kutoka idara ya maabara unafanyika katika vituo vya afya.
- Kuhakikisha uhifadhi salama wa vitu vinavyohusiana na Upimaji VVU na kuomba/kutayarisha vifaa vyote vya matumizi vinavyohitajika kwa huduma za Upimaji VVU.
- Kuweka Taarifa sahihi za upimaji VVU na kumbukumbu za rufaa/uhusiano (vitabu vya kumbukumbu, rejesta, ripoti).
- Kuandaa na kuwasilisha taarifa ya upimaji washirika wa ngono wa wapokea huduma za kila siku, kila juma na kila mwezi.
- Pia kuhakikisha taarifa ya upimaji VVU ya mwezi ni sahihi na inaingizwa kwenye DHIS2.
- Kuwasilisha mpango kazi wa juma kwa Mratibu wa magonjwa ya ngono, homa ya ini na UKIMWI wa Wilaya, pia kwa wasimamizi wa huduma za VVU katika jamii, msimamizi wa wilaya upnade wa mradi wa USAID Afya Yangu, msimamizi wa upimaji wa kituo cha afya husika Kwa usher na maelekezo.
- Kuwasilisha mpango kazi wa juma kwa Mratibu wa magonjwa ya ngono, homa ya ini na UKIMWI wa Wilaya, pia kwa wasimamizi wa huduma za VVU katika jamii, msimamizi wa wilaya upnade wa mradi wa USAID Afya Yangu, msimamizi wa upimaji wa kituo cha afya husika Kwa usher na maelekezo.
- Kuhakikisha ushirikiano kikazi na watumishi wa afya wa kituo, Mganga mfawidhi wa kituo, msimamizi wa kitengo cha huduma za matunzo na tiba ya VVU, wafanyakazi wa USAID Afya Yangu, timu za mikoa na halmashauri za usimamizi wa huduma za Afya, na wadau mbalimbali.
- Kupanga na kuwasilisha malengo ya ufanyaji kazi wa miezi 3 kwa ajili ya kupima utendaji kazi mwishoni mwa kipindi hicho.
- Kutoa huduma za uchunguzi wa magomvi baina ya wenza wa kingono (IPV) na kuwaunganisha waathirika kwenye huduma stahiki.
- Kufanya kazi na kuwa mshiriki wa timu ili kufuatilia mipango ya uboreshaji wa ubora kuhusiana na malengo/viashiria vya utendaji vilivyowekwa.
- Kuhakikisha upimaji wa VVU katika maeneo ya upimaji unafanywa kulingana na kanuni ya Kitaifa ya kupima VVU.
- Kushiriki kikamilifu katika mpango wa Kitaifa wa EQA wa upimaji wa haraka wa VVU.
- Kuandika anuani sahihi za makazi mwa wateja wapya.
- Kutekeleza majukumu mengine yoyote ambayo yanaweza kuhitajika na kiongozi wake kulingana na ujuzi na maarifa ya mtumishi.
MALENGO TARAJIWA
- Kuhakikisha upimaji wa VVU kwa washirika wa ngono wa wapokea huduma (Index Testing) unakubalika kwa zaidi ya asilimia 98 kwa wapokea huduma wapya (TX-NEW), wapokea huduma wenye idadi kubwa ya wingi wa VVU na wapokea huduma waliorudi kweye tiba baada ya kupotea (TX_RTT) wa mwezi husika.
- Kuhakikisha anawatambua na kuwapima washirika sahihi wa ngono wa wapokea huduma angalau wawili kwa kila mmoja.
- Kuhakikisha upimaji wa zaidi ya asilimia 98 kwa washirika wa ngono wa wapokea huduma waliotambulika.
- Kuhakikisha anawatambua na kuwapima angalau watoto watatu wa kibaiolojia wa wapokea huduma.
- Kuhakikisha upimaji wa zaidi ya asilimia 98 kwa watoto wa kibaiolojia wa wapokea huduma waliotambulika.
- Kufikisha malengo ya siku na mwezi ya upimaji VVU ikiwamo upimaji VVU kwa washirika wa ngono wa wapokea huduma, upimaji wa VVU unaoanzishwa na mtumishi wa afya, upimaji binafsi wa VVU, upimaji wa washirika wenye tabia sawa hatarishi kwa maambukizi ya VVU na dawa kinga kuzuia kupata maambukizi ya VVU (PrEP).
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe mwenye Elimu na Cheti cha Kidato cha nne (IV) na waliohitimu mafunzo ya Astashahada/ stashahada katika Fani ya Uuguzi/utabibu/maabara.
- Awe na leseni hai ya Kutoa Huduma (valid practice license), muombaji mwenye mafunzo na cheti cha upimaji VVU atapewa kipaumbele.
- Awe mwenye uzoefu wa kufanya kazi walau miezi sita katika vituo
vya Tiba na Matunzo vilivyopo Mkoani Njombe. - Awe na ujuzi wa uchambuzi na utatuzi wa changamoto.
Awe na uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili. - Awe muadilifu na mwenye uwezo wa kufanya kazi zinazohitaji utekelezaji wa haraka kwa usimamizi mdogo.
- Awe na uwezo wa kutunza siri na nyaraka za serikali katika nyanja zote.
- Awe na uwezo wa kutumia kompyuta – Microsoft Office kama Word, Excel, PowerPoint.
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini watu wa kuaminika.
- Maombi yote yaatambane na vyeti vya taaluma, nakala za vyeti vya
kidato cha nne, au sita kwa wale walifika kiwango hicho..Uwasilishaji wa taarifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za Kisheria. - Barua za maombi ziwasilishwe kwa Mkono kuletwa Masijala kwa njia
ya Posta au Mkono. - Watakachangulia kwa ajili ya usaili watajulishwa kwa simu.
- Waombaji ambao ni watumishi wa umma hawataruhusiwa kuomba nafasi hizi.
- Waombaji wawe wanaojitolea katika vituo vya kutolea huduma za afya na barua zao zipitishwe na wafawidhi wa vituo husika.
N.B: Posho ya kazi hii ya kujitolea italipwa na Mradi wa USAID Afya Yangu (My Health) Southern kwa kiwango cha TSH 400,000/= kwa mwezi.
Mwisho wa kupokea maombi ni 24 Januari, 2025.
