NAFASI 18 ZA KAZI KIGOMA DISTRICT COUNCIL
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka18 na usiozidi miaka 45
- Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
- Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao.
- Maombi yote yaambatane na nakala ya vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne/Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma.
- “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTSSLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
POST: MTENDAJI WA KIJIJI III – 8 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma More Details | 2024-10-11 Login to Apply |
POST: MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 4 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma More Details | 2024-10-11 Login to Apply |
POST: MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 3 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma More Details | 2024-10-11 Login to Apply |
POST: DEREVA DARAJA II – 3 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma More Details | 2024-10-11 Login to Apply |
