NAFASI 16 za Kazi Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Filed in Ajira by on 08/12/2024

NAFASI 16 za Kazi Wizara ya Mifugo na UvuviNAFASI 16 za Kazi Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Wizara ina jukumu la kusimamia na kuendeleza mifugo kwa ujumla na rasilimali za Uvuvi kwa ajili
ya kufikia Malengo ya Milenia, mkakati wa Taifa wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini, kuboresha maisha ya jamii zinazotegemea mifugo na uvuvi, usalama wa chakula bila kuathiri
ustawi wa Wanyama na uhifadhi wa mazingira, kujenga na kusaidia uwezo wa kiufundi na kitaaluma kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Sekta Binafsi ili kuendeleza, kusimamia na kudhibiti uendelevu wa rasilimali za mifugo na uvuvi.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

✅AFISA USIMAMIZI NYANDA ZA MALISHO II (RANGE MANAGEMENT OFFICER II)–NAFASI 4

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kubuni mbinu na miradi ya uendelezaji malisho na maji ya mifugo wilayani na kusimamia
    utekelezaji wake;
  • Kuratibu mipango ya ugani ya uendelezaji wa malisho;
  • Kufanya mafunzo ya uendelezaji malisho na vyanzo vya maji ya mifugo, kwa wataalam na
    wafugaji na wadau wengine;
  • Kufanya tafiti za rasilimali (Range resources survey) ya mifugo, vyakula vya mifugo, malisho
    na vyanzo vya maji;
  • Kusimamia na kudhibiti uharibifu wa mazingira katika maeneo ya nyanda za malisho katika wilaya;
  • Kushiriki katika shughuli za kudhibiti uvamizi wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ufugaji na
    njia za mifugo wilayani;
  • Kufuatilia, kuweka, kuchambua na kutafsiri takwimu za uendelezaji, matumizi na uhifadhi wa
    malisho wilayani;
  • Kufanya uchunguzi wa kina kuchora ramani za usambaaji wa mbung’o na ndorobo katika maeneo yao;
  • Kuhamasisha wananchi kushiriki katika njia/ mbinu bora na rahisi za kuzuia ndorobo.
  • Kutayarisha taarifa za robo, nusu na mwaka za uzuiaji wa mbung’o, Ndorobo, nagana, malale na hali ya malisho;
  • Kufanya kazi nyingine zozote za fani yake atakazoagizwa na kupangiwa na Mkuu wake

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Kwanza katika mojawapo ya fani ya Usimamizi wa Nyanda za Malisho (Range Management), Usimamizi wa Maliasili au Usimamizi wa Maeneo Kame kutoka chuo Kikuu cha Sokoine au sifa inayolingana na hiyo kutoka chuo kingine kinachotambulika na aserikali.

NGAZI YA MSHAHARA : TGS D

✅AFISA USIMAMIZI NYANDA ZA MALISHO MSAIDIZI DARAJA LA II (RANGE MANAGEMENT FIELD OFFICER II) NAFASI 4

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kufanya na kusimamia uchunguzi wa hali ya nyanda za malisho (trend), mbung’o na ndorobo
    katika eneo lake;
  • Kushirikiana na wahudumu wa nyanda za malisho kutembelea wafugaji na kuwapa ushauri
    fasaha wa kitaalam kuhusu uzalishaji na uhifadhi wa malisho katika eneo lake la kazi;
  • Kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya nyanda za malisho, vyakula vya ziada, maji ya mifugo na
    mbinu za uzuiaji wa mbung’o na ndorobo kwa wafugaji;
  • Kushauri na kuwaelekeza wafugaji na wadau wengine kuzalisha malisho na kuhifadhi malisho
    kwa kutumia njia mbalimbali kama hei/saileji/kutengwa yakiwa shambani bila kuchungwa;
  • Kukusanya na kutunza takwimu za malisho, mbung’o na ndorobo;
  • Kutayarisha ramani za usambaaji wa mbung’o na ndorobo katika eneo lake;
  • Kupanga na kusimamia shughuli zote za uzuiaji mbung’o na ndorobo katika eneo lake;
  • Kuhamasisha utumiaji wa mbinu salama za uzuiaji wa mbung’o na ndorobo kwa kuzingatia
    kanuni ya hifadhi ya mazingira;
  • Kufuatilia taarifa za awali za kuwepo kwa matukio ya ndorobo (nagana na malale).
  • Kuandaa taarifa za robo, nusu na mwaka za hali ya malisho na uzuiaji wa mbung’o na ndorobo;
    na
  • Kufanya kazi nyingine zozote za fani yake itakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au VI wenye Stashahada (Diploma-NTA Level 6) katika Nyanda za Malisho na Udhibiti wa Ndorobo kutoka Vyuo vya Wakala wa Mafunzo ya Mifugo (Livestock Training Agency – LITA) au sifa inayolingana na hiyo kutoka vyuo vingine vinavyotambuliwa na
Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: TGS C

✅MTEKNOLOJIA WA SAMAKI DARAJA LA II (FISH TECHNOLOGIST II) – Nafasi 7

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kutoa ushauri juu ya utayarishaji, uchakataji, ukaushaji na uhifadhi wa samaki na mazao ya uvuvi;
  • Kukagua na kusimamia ubora wa mazao ya uvuvi na mwani kulingana na viwango vya kitaifa
    ana kimataifa;
  • Kusimamia na kushauri kuhusu Kanuni za udhibiti ubora wa mazao ya uvuvi na mwani;
  • Kudhibiti ubora wa samaki katika mialo, masoko, viwanda na maghala;
  • Kudhibiti usafi katika maeneo ya kupokelea samaki na mwani;
  • Kukagua viwanda vinavyochakata, maghala ya kuhifadhia mazao ya uvuvi na vyombo vya usafirishaji wa mazao ya uvuvi kulingana na “HACCP” (Hazard Analysis Critical Control Point);
  • uhakiki nyaraka mbalimbali za uzalishaji na usafirishaji wa mazao ya uvuvi na mwani;
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wa Kitengo zinazohusiana na fani yake.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye mojawapo wa Shahada za fani za Fish Technology, Marine Biology and Applied Microbiology, Fisheries Sciences and Microbiology kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; Sayansi ya Chakula (Food Technology and Microbiology) kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine au sifa inayolingana na hiyo kutoka vyuo vikuu vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA : TGS D

✅MUUNDA BOTI DARAJA LA II (BOAT BUILDER II) – NAFASI 1

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kusaidia kuunda boti za uvuvi;
  • Kuwashauri wavuvi kuhusu utunzaji na matumizi ya boti;
  • Kufanya ukarabati wa boti;
  • Kusaidia kutafsiri/kusoma michoro ya kiufundi ya uundaji wa boti;
  • Kuandaa vifaa kwa ajili ya ujenzi wa boti; na
  • Kufanya kazi nyingine za fani yake kama atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV au VI wenye Stashahada (Diploma – NTA Level 6) ya Uundaji Boti kutoka Vyuo vya Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (Fisheries Education and Training
Agency – FETA) au sifa inayolingana na hiyo kutoka vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: TGS. C

MASHARTI YA JUMLA

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45.
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi yao na kuainisha vizuri
    kwenye dirisha la maombi uelemavu walionao kwa ajili ya utambuzi kwa Sekretarieti ya Ajira;
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyithibitishwa na
    Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia
    kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
    – Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
    – Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI Computer Certificate – Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
  • Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana
    kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa
    umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Muhimu: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu.
anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU, OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
S.L.P. 2320 DODOMA.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;http://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya
Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 17th Desemba, 2024.


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Comments are closed.

error: Content is protected !!