NAFASI 141 Za Tabibu Msaidizi MDAs & LGAs

NAFASI 141 Za Tabibu Msaidizi MDAs & LGAs
NAFASI 141 Za Tabibu Msaidizi MDAs & LGAs
✅TABIBU MSAIDIZI DARAJA LA II (CLINICAL ASSISTANT II) NAFASI – 141
MAJUKUMU YA KAZI
- Kutoa huduma za kinga na tiba;
- Kutambua na kutibu magonjwa;
- Kutoa huduma ya Afya ya msingi (Primary Health Care);
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Taifa wa Kidato cha IV ambao wamehitimu Mafunzo ya Miaka Miwili ya Tabibu (Clinical Assistants Certificate).
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali TGHS A
MASHARTI YA JUMLA.
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini;
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu
walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma; - Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili - Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombiya
nafasi za kazikwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo. - Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina yawadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato
cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
– Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
– Computer Certificate
– Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards) - “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo zakidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi
kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi. - Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba,
2010. - Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamojana vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320, DODOMA.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;http://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa‘Recruitment Portal’)
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika
tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 20 Januari, 2025.
POST: TABIBU MSAIDIZI II (CLINICAL ASSISTANT II) – 141 POST Employer: MDAs & LGAs More Details | 2025-01-20 Login to Apply |
