NAFASI 14 ZA KAZI KAKONKO DISTRICT COUNCIL
NAFASI 14 ZA KAZI KAKONKO DISTRICT COUNCIL
- Afisa Masuuli na mtendaji mkuu wa Serikali ya Kijiji;
- Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika Kijiji;
- Kuratibu na kusimamia upangaji wa mipango ya maendeleo ya Kijiji;
- Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya Kijiji;
- Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
- Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha Wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali;
- Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya kitaalamu katika Kijiji;
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji;
- Mwenyekiti wa kikao cha wataalamu waliopo katika Kijiji;
- Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
- Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za Kijiji; na
- Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
- Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali; na
- Kufanya usafi wa Gari;
- Kuorodhesha baruazinazoingia masijala mwenye regista (Incoming Correspondence Register), Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (Outgoing Correspondence Register).
- Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers)
- Kupokea majalada yanayorudi masijala kutoka kwa watendaji
- Kutafuta kumbukumbu/ Nyaraka au majalada yanayohitajika na watendaji, Kurudisha majalada kwenye shubaka/ kabati la majalada (Racks/Filling Cabinets) au Mahali pengine yanapohifadhiwa.
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi (File tracking)
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri
- Kupokea Wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
- Kutunza taarifa za kumbukumbuka za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine.
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
- Kupokea majalada na kusambaza kwa Maafisa walio katika Idara/ Kitengo/ sehemu husika.
- Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi
- Kufanya kazi nyingine atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
- Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania wenye umri wa Kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya Ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani, namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) wakuaminika.
- Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao.
- Maombi yote yaambatane na nakala ya vyeti vya Elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili ambavyo ni vyeti vya kidato cha Nne/ Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Diploma/Certificate, Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, Computer Certificate, Vyeti vya Kitaaluma.
- Testimonials, “Provision Results”, “Statements of Results”, hati ya matokeo ya kidato cha Nne na Sita HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya nchi wa hakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushiwa husika watachukuliwa hatua za kisheria
POST: MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – 5 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko More Details | 2024-09-30 Login to Apply |
POST: MTENDAJI WA KIJIJI III – 5 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko More Details | 2024-09-30 Login to Apply |
POST: MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – 2 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko More Details | 2024-09-30 Login to Apply |
POST: DEREVA DARAJA II – 2 POST Employer: Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko More Details | 2024-09-30 Login to Apply |
