NAFASI 10 ZA KAZI KAKONKO DISTRICT COUNCIL
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko anayo furaha kutangaza nafasi 10 za ajira ya Vibarua kwa watanzania wote wenye sifa stahiki kwa nafasi ya Vibarua wa usafi nafasi 8 na Waingiza Taarifa katika mfumo wa TASAF MIS nafasi 2.
- Kufanya usafi wa ndani
- Kufanya usafi wa nje
- Kuandaa kumbi za mikutano
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
- Awe anajua kusoma na kuandika
- Muombaji awe na umri kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45
- Muombaji awe mchapakazi.
- Muombaji awe muadilifu
- Jukumu Kubwa ni Kuingiza data kwenye Mfumo TASAF MIS
- Kuingiza taarifa za kaya (Data Update)
- Kusajiri Miradi ya PWP
- Kuingiza taarifa za Mahudhurio ya walengwa waliofanya kazi (mahudhurio ya kazi)
- Kuingiza taarifa za walengwa kwa ajili ya kutimiza masharti ya Elimu na Afya Kusajili vikundi vya COMSIP
- Kuingiza taarifa za fedha kwa wanavikundi vya kuweka akiba na kuwekeza na Uncollected
- Kuingiza mipango kazi ya Biashara na Taarifa za malipo za walengwa Pamoja na majukumu mengine utakayopangiwa na mkuu wako wa kazi
- Wahitimu wa kidato cha nne
- Awe ana ujuzi wa kutumia Komputya Muombaji awe mchapakazi
- Muombaji awe muadilifu
