NAFASI 10 za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Kigoma

Filed in Ajira by on 30/11/2024 0 Comments

NAFASI 10 za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni KigomaNAFASI 10 za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Kigoma

Mganga Mfawidhi Wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Kigoma anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kai katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni uwepo wa nafasi 10 za mkataba wa kujitolea kwa kada mbalimbali kama ilivyo ainishwa hapo chini.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Nafasi za kazi zinazotangazwa ni kama ifuatavyo:-

✅Dereva II TGS B-(Nafasi 2)

Sifa za mwombaji: –

  • Waombaji wawe na cheti cha kidato cha nne (Form IV) na Leseni ya Daraja la E au C1 ya uendeshaji Magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
  • Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi stadi (VETA), NIT au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

Kazi za kufanya:-

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari,
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi,
    Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari,
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali,
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari, Kufanya usafi wa gari, na
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake

✅Mteknolojia mionzi (Radiographer) II – TGHS B (Nafasi 3)

Sifa za mwombaji;

  • Awe na diploma au shahada ya sayansi ya mionzi (Radiologic Technology) kutoka chuo kinachotambulika na selikari
  • Awe na Leseni ya kitaaluma kutoka bodi husika, kama Baraza la Wataalamu wa Afya

Uzoefu na Ujuzi:

  • Mwenye Uzoefu wa kufanya kazi katika nyanja ya mionzi au hospitalini.
  • Mwenye Uwezo wa kutumia vifaa vya kisasa vya mionzi kama X-ray, CT scan, MRI, na Ultrasound.
  • Maarifa ya kiusalama kuhusu mionzi na uwezo wa kufuata kanuni za kiafya.

Kazi za Mteknolojia wa mionzi

  • Kufanya uchunguzi wa mionzi ili kusaidia madaktari kugundua matatizo ya kiafya kama vile mifupa iliyovunjika, uvimbe, na magonjwa mengine.
  • Kufanya uchunguzi kwa kutumia vifaa maalum kama vile:
    Mashine za X-ray.
  • CT (Computed Tomography) Scan.
  • MRI (Magnetic Resonance Imaging).
    Ultrasound.
  • Kuchambua na kuwasilisha picha za mionzi kwa madaktari ili kusaidia kutoa matibabu bora.
  • Kuandaa wagonjwa kwa uchunguzi kwa kuwaeleza mchakato wa uchunguzi na kuwahakikishia usalama wao.
  • Kusimamia na kudumisha vifaa vya mionzi kuhakikisha vinafanya kazi vizuri na kwa usalama.

✅Muuguzi Wa Usingizi (anaesthesia Nurse) – Nafasi 3
Waombaji wawe na stashahada ya uuguzi wenye mafunzo maalum ya anesthesia (utoaji wa dawa za usingizi) na vyeti vinavyotambulika katika taaluma husika.

Majukumu ya Muuguzi wa Usingizi

  • Kufanya kazi na vifaa vya kisasa vya anesthesia, kama mashine za kutoa dawa za usingizi na vifaa vya kufuatilia hali ya mgonjwa.
  • Awe na Uelewa mzuri wa anatomia, fiziolojia, na farmakolojia, hasa kuhusu dawa za usingizi na athari zake kwa mwili wa binadamu.
  • Kuchambua viashiwa muhimu vya mgonjwa (mapigo ya moyo, shinikizo la damu, n.k.) na kuchukua hatua stahiki haraka ikiwa hali itabadilika.
  • Kudhibiti mazingira ya dharura kama mgonjwa anapopata matatizo ya kiafya wakati wa usingizi wa dawa.
  • Pamoja na kazi zingine za kitaaluma ambazo ataelekezwa na kiongozi/mwajiri wake

✅Msaidizi wa Kumbukumbu II TGS C – (Nafasi 1)

Sifa za Mwombaji: –
Waombaji wawe wahitimu wa kidato cha nne au sita wenye Stashahada ya utunzaji kumbukumbu kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma au chuo chochote kinachotambulika na serikali.

Kazi za kufanya za Msaidizi wa Kumbukumbu: –

  • Kutafuta kumbukumbu/ nyaraka/mafaili yanayohitajika na wasomaji.
  • Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka.
  • Kuweka/kupanga kumbukumbu/ nyaraka Katika reki (file racks/cabinets) katika masjala/ vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
  • Kunukuu (kurekodi) mwenendo mzima wa nyaraka na kuweka kumbukumbu sahihi za nyaraka zinazoingia masjara.
  • Kuhakiki na kuandaa taarifa iliyohakikiwa na kuwasilisha sehemu husika kabla yakutoa nakala kwa Umma.
  • Kufanya kazi zingine kama itakavyoamuliwa au kuelekezwa na kiongozi wake au msimamizi wake wa kazi.

✅Mhudumu wa Chumba Cha Kuhifadhi Maiti – TGHOS-A (Nafasi 1)

Sifa za Mwombaji.
Muombaji awe na elimu ya kidato cha nne na aliyehitimu mafunzo maalumu ya mwaka mmoja ya uhudumu wa chumba cha kuhifadhi miili (mortuary attendant) kutoka chuo kinachotambulika na serikali.

Kazi za Mhudumu wa Chumba cha Kuhifadhi maiti

  • Kufanya usafi wa chumba cha kuhifadhia maiti
  • Kazi nyingine atakazopangiwa na kiongozi wake wa kazi
    Kupokea, kuosha na kutunza maiti.

Sifa za Jumla za Waombaji

  • Awe Raia wa Tanzania;
  • Awe na Umri usiopungua miaka 18 na usiozidi Umri wa miaka 45;
  • Asiwe Mwajiriwa wa Serikali.
  • Kila mwombaji aambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho wa taifa (NIDA).
  • Waombaji watakaokidhi vigezo wataitwa kwenye usaili na watakaoshindwa kuzingatia masharti ya tangazo hili hawataitwa.
  • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi (CV), akionesha namba za simu na anuani yake na wadhamini 3 wa uhakika, vyeti vya elimu na taaluma.
  • Mwombaji awe na uzoefu usio pungua miaka mitatu (3) katika taaluma hiyo akiwa anafanya kazi, hivyo waombaji wenye uzoefu wa muda mrefu watapewa kipaumbele.
  • Barua za maombi ziwasilishwe Pamoja na nyaraka zingine kama PDF File. Pia waombaji watakao tuma maombi yao nje ya muda na utaratibu maombi yao hayatafanyiwa kazi.

Sifa za Kitaaluma.
Waombaji wote wawe na vyeti vya elimu, vyeti vya taaluma, leseni kwa waombaji ambao wamesajiriwa na baraza la taaluma husika..

Mshahara na Marupurupu.
Waombaji watakaopata nafasi na kupewa mkataba watalipwa kwa kuzingatia Mwongozo wa kufanya kazi kwa kujitolea wa wizara ya Afya wa mwaka 2021.

Maombi yote yaambatanishwe na: –

  • Nakala ya cheti cha kuzaliwa;
  • Nakala ya cheti cha Kidato cha Nne au/na cha Sita kulingana na Kada ya Mwombaji:
  • Nakala ya Vyeti vya Taaluma (Cheti na Transcripts) na Wasifu (C.V);
  • Picha ndogo (passport size) mbili za hivi karibuni.

NB:
Waombaji waambatanishe barua ya maombi na viambata vingine muhimu kwa Pamoja kama PDF na vinginevyo.

Maombi yote yatumwe Kwa njia ya barua pepe (barua@mawenirrh.go.tz), au yapelekwe OFISI YA MGANGA MFAWIDHI kuanzia Tarehe 29/11/2024 hadi Tarehe 05/12/2024 Saa 09.30 alasiri.

Maombi yote yaelekezwe kwa;
Mganga Mfawidhi,
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni,
S.L.P 16,
KIGOMA


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!