Mwongozo wa Ujazaji Nyaraka Ajira za Jeshi la Uhamiaji
Mwongozo wa Ujazaji Nyaraka Ajira za Jeshi la Uhamiaji
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kwa Mamlaka aliyonayo chini ya Kanuni Namba 11(1) ya Kanuni za Uendeshaji za Uhamiaji za Mwaka 2018, November 30, 2024 ametangaza nafasi za Ajira Mpya za Askari wa Uhamiaji kwa Vijana wa Kitanzania wenye sifa zilizoainishwa kwenye Tangazo husika.
Katika uombaji wa Ajira hizo Nijuze Habari tumekuwekea hapa hatua kwa hatua na namna ya kujaza Nyaraka zilizoainishwa hapa chini;
Wakati wa kufanya Maombi, Mwombaji anatakiwa kuambatisha (upload) kwenye
mfumo wa Ajira nyaraka zilizo katika mfumo wa PDF na picha ya mwombaji
(passportsize) katika mfumo wa jpg/png na kila Nyaraka moja isizidi ukubwa wa
300Kb.
Orodha ya nyaraka hizo ni kama ifuatavyo;
- Nakala ya Cheti cha Kuzaliwa
- Awe na namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) kwa ajili ya kujisajili
kwenye mfumo. - Barua ya maombi ya ajira iliyoandikwa kwa mkono.
- Barua ya Utambulisho toka Serikali ya Mtaa/Kijiji au Shehia; kwa walio Makambini JKT/JKU wawe na barua za Utambulisho kutoka kwa Mkuu wa Kambi.
- Picha (passport size) ya hivi karibuni iliyo katika mfumo wa jpg/png na isiyozidi 300kb
- Awe na namba (index no) ya cheti cha Kidato cha Nne na Sita kwa
waliohitimu kidato hicho ambapo atajaza namba hizo kwenye mfumo wa ajira. - Nakala ya vyeti vya kuhitimu fani mbalimbali ngazi ya Astashahada,
Stashahada, na Shahada/ Stashahada ya Juu (kama anavyo na viwe vimehakikiwa katika vyuo husika). - Nakala ya cheti cha kuhitimu JKT/JKU(kwa walionavyo).
- Vyeti vya usajili wa taaluma kwa fani zinazohitaji usajili wa Bodi
- Wasifu wa Mwombaji (CV).

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Tags: Mwongozo wa Ujazaji Nyaraka Ajira za Jeshi la Uhamiaji