MWONGOZO WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024

Filed in Makala by on 10/09/2024 0 Comments
MWONGOZO WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024

MWONGOZO WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024

Mwongozo huu wa Uchaguzi wa viongozi wa Vitongoji, Vijiji na Mitaa umeandaliwa kwa lengo la kufafanua kwa lugha rahisi maudhui ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika ngazi za msingi.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Kwa mujibu wa mwongozo huu ngazi za msingi za Serikali za mitaa zina maana ya Mitaa katika
Mamlaka za Miji, Vijiji na Vitongoji katika Mamlaka za Wilaya na Mamlaka za Miji zenye Vijiji na Vitongoji.

Kwa kufafanua kwa lugha rahisi mwongozo huu utawasaidia, Wasimamizi, Wasimamizi Wasaidizi, Wasimamizi wa Vituo vya Uchaguzi na Wadau wengine wa Uchaguzi kufahamu majukumu yao katika kusimamia mchakato mzima wa Uchaguzi.

Aidha, Mwongozo huu utawawezesha wadau wa Uchaguzi, pamoja na mambo mengine, kufahamu haki na wajibu wa vyama vya siasa na wapiga kura.

Ni mategemeo ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuwa, kupitia Mwongozo huu, Uchaguzi utafanyika katika mazingira huru, uwazi, amani na haki kwa washiriki wote. OR – TAMISEMI

kama Mamlaka ya Uchaguzi inatarajia kuwa Wasimamizi, Wasimamizi Wasaidizi, Wasimamizi wa Vituo, Mawakala na Wadau wengine wote wa Uchaguzi watashiriki katika shughuli za Uchaguzi wakizingatia maslahi mapana ya nchi yetu ikiwa ni pamoja na kudumisha demokrasia na kuimarisha amani, utulivu, mshikamano na umoja wa kitaifa.

Pamoja na kufafanua Kanuni za Uchaguzi kwa lugha rahisi, Mwongozo huu umejumuisha pia mtiririko wa matukio ya Uchaguzi kuanzia tarehe ya Tangazo la Uchaguzi hadi tarehe ya Uchaguzi.

Ratiba ya Uchaguzi imefanywa kuwa ni sehemu ya Mwongozo huu ili kurahisisha rejea.

MWONGOZO WA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA NGAZI ZA VIJIJI, VITONGOJI NA MITAA 2024 DOWNLOAD PDF

SOMA 

RATIBA YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!