Mustafa Kodro Kocha Msaidizi Young Africans
Mustafa Kodro Kocha Msaidizi Young Africans
Klabu ya Young Africans imemtambulisha Mustafa Kodro kuwa Kocha Msaidizi wa kikosi cha mabingwa hao wa nchi akichukuwa nafasi iliyoachwa na Moussa N’Daw
Kodro mwenye umri wa miaka 43 ni pendekezo la Kocha Mkuu, Sead Ramovic ambaye alifanya naye kazi katika klabu ya TS Galaxy ya Afrika Kusini

Mustafa Kodro Kocha Msaidizi Young Africans
Kodro ambaye ni raia wa Bosnia ana leseni ya ukocha ya UEFA Pro.
Kabla ya kuingia kwenye ukocha, Kodro alikuwa kiungo mahiri akicheza katika klabu mbalimbali za Premia Ligi nchini kwao Bosnia.
Kodro anakamilisha benchi la ufundi la Young Africans ambalo linawajumuisha wataalam wote waliobaki ambao walikuwa katika benchi la Miguel Gamondi ukimuondoa Moussa Ndaw.
