MFUMO wa Maombi ya Ajira Kada ya Afya

Filed in Makala by on 06/12/2024

MFUMO wa Maombi ya Ajira Kada ya AfyaMFUMO wa Maombi ya Ajira za Afya

Tumia namba ya NIDA au barua pepe uliyotumia kujisajili kama jina la mtumiaji (username)MFUMO wa Maombi ya Ajira za Afya
Maelekezo.
  • Tafadhali chagua aina ya maombi ya ajira ambayo ni AFYA.
  • Kama ni muombaji mpya bofya kiunganishi cha juu kulia “Jisajili” kuanza kuomba
  • Ingiza namba ya NIDA au barua pepe kama jina la mtumiaji na uingize nywila yako kuingia ndani ya mfumo.
  • Baada ya kufanikiwa kuingia ndani, tafadhali kamilisha maombi yako kabla ya tarehe ya mwisho
  • Maombi yasiyokamilika hayatafanyiwa kazi
  • Hakikisha kabla ya kutuma maombi umesoma na kuelewa vizuri tangazo lilotolewa
  • Hakikisha vyeti ulivyo ambatanisha vinasomeka vizuri
  • Kuwasilisha taarifa za kughushi zitapelekea kuchukuliwa hatua za kisheria dhidi yako.

BONYEZA HAPA KULOGIN

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

BOFYA HAPA KUJISAJILI KWAAJILI YA KUTUMA MAOMBI

Waombaji waliowahi kutuma maombi yao awali kupitia mfumo huu wanatakiwa kuhuisha taarifa zao na barua za maombi.

Waombaji wote wanatakiwa kuwa na sifa za jumla kama ifuatavyo:

  • Awe raia wa Tanzania;
  • Awe na umri usiozidi miaka 45;
  • Awe na vyeti kamili vya mafunzo ya fani aliyosomea (Cheti cha Kidato cha Nne, Sita, Taaluma na usajili kamili (Full Registration) au Leseni hai ya kufanya kazi ya taaluma husika);
  • Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au Mwajiriwa wa Hospitali za Mashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwa na Serikali;
  • Kwa waombaji waliosajiliwa na mabaraza ya taaluma ni lazima awe na Leseni hai kutoka Baraza la taaluma yake
  • Awe hajawahi kufukuzwa, kuacha kazi au kustaafishwa katika Utumishi wa Umma;
  • Kitambulisho cha Taifa (NIDA); na
  • Aambatishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.

Mambo Muhimu ya Kuzingatia kwa Waombaji wote

  • Waombaji wote wawe tayari kufanya kazi katika Halmashauri yeyote watakayopangiwa
  • Waombaji wote wahakikishe wanajaza taarifa zao na kuambatisha nyaraka zote muhimu kwenye mfumo; na Maombi ya ajira hizi ni bure.

Kwa Msaada
Tafadhali piga simu huduma kwa mteja :026-2160210 au 0735-160210

TAZAMA HAPA AJIRA MPYA 400 KADA YA AFYA DECEMBER 2024


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Comments are closed.

error: Content is protected !!