MFAHAMU Donald Trump rais wa 47 wa Marekani

Filed in Makala by on 06/11/2024 0 Comments

MFAHAMU Donald Trump rais wa 47 wa MarekaniMFAHAMU Donald Trump rais wa 47 wa Marekani

Trump ameibuka mshindi baada ya kumshinda mpinzani wake kutoka chama cha Democrats bi Kamala Harris

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mgombea huyo wa Republican alipata ushindi mnono dhidi ya Kamala Harris, unaomruhusu kurejea katika kiti cha urais wa Marekani.

Trump, ambaye alishinda uchaguzi wa 2016 na kupoteza ule wa 2020, alichukua uongozi mbele ya Harris, ambaye alichukua nafasi ya Joe Biden kama mgombeaji wa Democrats zaidi ya siku 100 zilizopita.

Miaka mingi nyuma kabla ya kugombea mara tatu mfululizo kuwania urais wa Marekani, Donald Trump mwenye umri wa miaka 78 alikuwa bilionea mwenye mbwembwe nchini Marekani.

Maisha ya tajiri huyo wa majengo huko New York yalikuwa kwenye magazeti ya udaku na runinga katika miongo kadhaa kabla ya mbio zake zisizotarajiwa za 2015-16 kuingia Ikulu ya White House.

Jina lake na mtindo wake wa kampeni – vilimsaidia kuwashinda wanasiasa wenye uzoefu – lakini enzi iliyojaa utata ilimfanya aondolewe madarakani kwa kura baada ya muhula mmoja.

Mrithi wa Baba yake

getty

Chanzo cha picha,Getty Images

Trump ni mtoto wa nne wa mfanyabiashara wa majengo huko New York, Fred Trump. Alipelekwa katika shule ya kijeshi akiwa na umri wa miaka 13 alipoanza utovu wa nidhamu shuleni.

Baada ya kupata digrii ya awali kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylvania, alionekana kuwa ndiye kumrithi wa baba yake, wakati kaka yake mkubwa, Fred, alipochagua kuwa rubani.

Fred Trump alifariki akiwa na umri wa miaka 43 kutokana na ulevi wa kupindukia, jambo ambalo Trump anasema lilimpelekea kuepuka pombe na sigara maisha yake yote.

Trump anasema aliingia kwenye biashara ya majengo akiwa na mkopo wa dola za kimarekani milioni 1 kutoka kwa babake kabla ya kujiunga na kampuni hiyo.

Alisaidia kusimamia miradi ya makazi ya baba yake katika mitaa ya Jiji la New York, na kuchukua udhibiti wa kampuni hiyo – ambayo aliipa jina la Trump Organisation – mwaka 1971.

Baba yake, ambaye Trump anamtaja kama “msukumo wangu,” alifariki mwaka 1999.

Biashara za Trump

rrr

Chanzo cha picha,Getty Images

Chini ya Trump, biashara ya familia ilihama kutoka majengo ya makazi ya kuishi huko Brooklyn na Queens hadi miradi ya Manhattan.

Mtaa maarufu wa Fifth Avenue ukawa makazi ya ghorofa la Trump Tower, bila shaka ndiyo jengo maarufu la tajiri huyo na nyumba yake kwa miaka mingi. Na hoteli ya Commodore ikaitwa Grand Hyatt.

Majengo mengine yenye jina la Trump – kama makasino, ghorofa za makazi, viwanja vya gofu na hoteli – yalijengwa pia, huko Atlantic City, Chicago na Las Vegas, India, Uturuki na Ufilipino.

rrr

Chanzo cha picha,Getty Images

Kuibuka kwake kuwa maarufu kuliendelea katika ulimwengu wa burudani – kwanza kama mmiliki wa shindano la Miss Universe, Miss USA, na Miss Teen USA, kisha kama mtayarishaji wa kipindi cha NBC The Apprentice.

Trump ameandika vitabu kadhaa, alionekana katika filamu na programu ya kuunga mkono mieleka, na alikuwa muuzaji wa kila kitu kutoka vinywaji hadi tai. Lakini utajiri wake umeshuka katika miaka ya hivi karibuni. Forbes inakadiria kuwa kwa sasa ana utajiri wa dola za kimarekani bilioni 4.

Trump pia ametangaza kufilisika kwa biashara kadhaa kwa nyakati sita tofauti, ikiwa ni pamoja na mradi wa Trump Steaks na Chuo Kikuu cha Trump.

Pia ameficha taarifa zake kuhusu ushuru ili zisichunguzwe, na ripoti ya 2020 ya gazeti la New York Times lilifichua miaka ya kukwepa ushuru wa mapato na upoteaji wa fedha.

Familia yake

Maisha ya binafsi ya Trump yako hadharani. Mke wake wa kwanza, anayejulikana zaidi, ni Ivana Zelnickova, mwanariadha wa Czech na mwanamitindo. Wamepata watoto watatu – Donald Jr, Ivanka na Eric – kabla ya talaka mwaka 1990.

Kesi yao mahakamani ilikuwa kwenye kurasa za mbele za magazeti ya udaku, na madai ya marehemu Bi Trump ya kunyanyaswa – ambayo baadaye aliyapuuza katika makala ya runinga kuhusu Trump.

Alimwoa mwigizaji Marla Maples mwaka 1993, miezi miwili baada ya kuzaliwa mtoto wao pekee Tiffany. Waliachana mwaka 1999.

Mke wa sasa wa Trump ni mwanamitindo wa zamani wa Slovenia, Melania Knauss. Walifunga ndoa mwaka 2005 na wana mtoto wa kiume, Barron William Trump, ambaye hivi karibuni ametimiza miaka 18.

Madai ya utovu wa maadili na uchepukaji nje ya ndoa yamemwandama Trump.

Mapema mwaka huu, majaji wawili tofauti walimpata Trump na hatia ya kumkashifu mwandishi E Jean Carroll katika juhudi za kukanusha shtaka la unyanyasaji wa kijinsia. Aliamriwa kumlipa dola milioni 88, lakini amekata rufaa.

Trump pia alipatikana na hatia kwa makosa 34 ya kughushi rekodi za biashara katika malipo ya pesa za kumnyamazisha mwigizaji wa filamu za ngono Stormy Daniels, juu ya madai ya kutoka naye nje ya ndoa mwaka 2006.

Mgombea urais

getty

Chanzo cha picha,Getty Images

Katika mahojiano ya 1980, Trump mwenye umri wa miaka 34 anaelezea siasa ni “maisha duni” na kusema “watu wenye uwezo” huchagua ulimwengu wa biashara.

Kufikia 1987, alianza kueleza hamu ya kuwania urais. Alichunguza uwezekano wa kuingia katika mbio za urais 2000 na kupitia Chama cha Reform, na chama cha Republican mwaka 2012.

Trump alikuwa miongoni mwa waumini wa nadharia ya “birtherism,” nadharia inayohoji iwapo Barack Obama alizaliwa Marekani. Hakukubali kuwa nadharia hiyo ni ya uwongo hadi 2016, lakini hakuwahi kuomba msamaha.

Juni 2015 Trump alitangaza rasmi mbio za Ikulu ya White House. Katika hotuba ya awali alionyesha utajiri wake na mafanikio ya biashara; akaishutumu Mexico kwa kuleta dawa za kulevya, uhalifu na wabakaji Marekani; na, kuahidi kuifanya nchi hiyo kulipia ujenzi wa ukuta katika mpaka.

Mijadala na sera zilizojaa utata vilivutia wafuasi na wakosoaji kwa kiwango sawa, pamoja na kufuatiliwa na vyombo vya habari.

Chini ya kauli mbiu ya ‘Make America Great Again’, aliwashinda wapinzani wake katika Chama cha Republican kwa urahisi na kukabiliana na Hillary Clinton wa Democrat.

Kampeni zake zilikumbwa na utata, ikiwa ni pamoja na kuvuja kwa kanda ya sauti yake akijigamba kuhusu unyanyasaji wa kijinsia, na alikuwa nyuma katika kura za maoni wakati wote wa uchaguzi mkuu.

Lakini Trump ndiye aliyecheka mwisho dhidi ya wachambuzi na wadadisi kwa ushindi wake wa kushangaza dhidi ya Hillary. Aliapishwa kuwa rais wa 45 wa nchi hiyo tarehe 20 Januari 2017.

Rais

Getty

Chanzo cha picha,Getty Images

Kutoka masaa machache tu tangu aanze kazi, vituko vikaibuka – akitoa matangazo rasmi kwenye Twitter (sasa X) na kugombana waziwazi na viongozi wa kigeni.

Alijiondoa katika mikataba ya mabadiliko ya tabia nchi na biashara, akapiga marufuku watu kutoka nchi saba zenye Waislamu wengi kuingia Marekani, akaweka vikwazo vingine vikali katika uhamiaji, akaanzisha vita vya kibiashara na China, akatekeleza sera ya kupunguza kodi, na kurekebisha uhusiano wa Mashariki ya Kati.

Kwa takriban miaka miwili, mchunguzi maalumu alichunguza madai ya kula njama ya timu ya kampeni ya Trump ya 2016 na Urusi. Watu 34 walikabiliwa na mashtaka ya uhalifu – kuhusu masuala kama vile udukuzi wa kompyuta na uhalifu wa kifedha – lakini sio Trump.

Baadaye, Trump akawa rais wa tatu wa Marekani katika historia kushtakiwa, kwa tuhuma za kuishinikiza serikali ya kigeni kufichua machafu ya mpinzani wake Joe Biden. Alipigwa kura ya kutokuwa na imani naye na Bunge linaloongozwa na Democrat, lakini kura hiyo haikupita katika Seneti inayoongozwa na Republican.

Mwaka wa uchaguzi wa 2020 ulitawaliwa na janga la Uviko 19.

Mbio za Kurudi Ikulu

Maisha ya kisiasa ya Trump yalionekana kama yamekufa baada tukio la Capitol. Wafadhili na wafuasi waliapa kutomuunga mkono tena, na hata washirika wake wa karibu walimkataa hadharani.

Hakuhudhuria kuapishwa kwa mrithi wake na akaihamishia familia yake Florida. Lakini akiwa na jeshi la wafuasi watiifu, aliendelea kuwa na ushawishi mkubwa katika Chama cha Republican.

Urithi wa urais wake uliibuka tena baada majaji watatu wa mrengo wa kulia ambao aliwateua kwenye Mahakama ya Juu – walipoondosha sheria ya takribani miaka 50 ya haki ya kitaifa ya utoaji mimba.

Licha ya kulaumiwa kwa matokeo mabaya ya chama cha Republican katika uchaguzi wa katikati ya muhula wa 2022, Trump alitangaza kuwania tena urais na kisha akawa kinara wa chama hicho.

Zaidi ya wagombea kumi, akiwemo makamu wake wa zamani wa rais, walishindana naye lakini akashinda kwani Trump alikwepa mijadala nao na kuelekeza hasira zake kwa Biden.

Trump alianza mbio za kuelekeza uchaguzi mkuu akikabiliwa na mashtaka 91 ya uhalifu katika kesi nne za jinai lakini mkakati wake wa kuchelewesha kesi hizo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Kesi tatu sasa hazitasikilizwa hadi uchaguzi upite, na hukumu ya kesi nyingine huko huko New York – imecheleweshwa hadi mwishoni mwa Novemba.

Tarehe 13 Julai, kijana mwenye bunduki mwenye umri wa miaka 20 alijaribu kumuua Trump wakati wa mkutano wa kampeni huko Butler, Pennsylvania. Thomas Matthew Crooks alifyatua risasi nane kutoka juu ya paa la karibu, na kumjeruhi Trump katika sikio lake la kulia kabla ya mshambuliaji huyo kuuawa.

Siku kadhaa baadaye, kwenye Kongamano la Kitaifa la Republican, chama hicho kilimsifu na kumtawaza rasmi kuwa mgombea urais wa Republican kwa mara ya tatu mfululizo, na kuanzisha pambano la marudiano dhidi ya Biden.

Tangu Biden ajiuzuru na kumuunga mkono naibu wake, Kamala Harris, Trump amejaribu kumfungamanisha na kushindwa kwa utawala wa Biden.

Trump amewaambia wafuasi wake kwamba tarehe 5 Novemba 2024 – tarehe ya uchaguzi wa Marekani – itakuwa “tarehe muhimu zaidi katika historia ya nchi yetu.”

Chanzo Cha Habari: BBC Swahili


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!