MATOKEO ya Uchaguzi Mkuu Chadema 2025

Filed in Habari by on 22/01/2025 0 Comments
MATOKEO ya Uchaguzi Mkuu Chadema 2025

MATOKEO ya Uchaguzi Mkuu Chadema 2025

MATOKEO ya Uchaguzi Mkuu Chadema 2025

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Breaking: Tundu Lissu ndiye Mwenyekiti mpya Chadema Taifa.

Tundu Lissu amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akimshinda mtangulizi wake, Freeman Mbowe aliyekuwa anatetea nafasi yake katika uchaguzi wa kihistoria uliofanyika January 21,2025 katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Katika uchaguzi huo Mbowe amepata kura 482 na Tundu Lissu kura 513.

Uchaguzi huu unafunga ukurasa wa miaka kadhaa ya uongozi wa Mbowe, ambaye ameiongoza CHADEMA kwa kipindi kirefu na aliyejizolea umaarufu mkubwa kama nguzo kuu ya upinzani nchini Tanzania.

Lissu, ambaye amejizolea umaarufu mkubwa baada ya kurejea kutoka uhamishoni na kuwa kiongozi shupavu katika upinzani, ameongoza kampeni ya kushinda nafasi hiyo.

Hata hivyo, Mbowe amekubali matokeo kwa heshima, akimpongeza Lissu na kusema anajiandaa kuunga mkono uongozi wake mpya.

Kupitia ukurasa wake wa Mtandao kijamii wa X, Mbowe ameandika ujumbe wa kukubali kushindwa akiandika kuwa;

“Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya Uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi 22 Januari 2025. Nampongeza Mhe. Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la Uongozi wa Chama”, ameandika Freeman Mbowe

Kuchaguliwa kwa Lissu kunakuja wakati muhimu kwa CHADEMA, ikiwa ni sehemu ya mabadiliko makubwa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

Lissu anaonekana kama kiongozi mwenye mvuto na msimamo mkali dhidi ya utawala wa sasa, na chama kinatarajia kuimarika zaidi chini ya uongozi wake.

Kwa upande wa Mbowe, kumaliza kwa uongozi wake ni ishara ya demokrasia ndani ya CHADEMA, ambapo mabadiliko ya kisiasa yanapatikana kwa njia ya amani na heshima.

Baada ya kutangazwa matokeo hayo ya uchaguzi mwenyekiti mpya wa Chadema, Tundu Lissu amemshukuru mtangulizi wake Freeman Mbowe na kueleza kuwa walichofanya kitaacha historia kwenye siasa za Tanzania.

Lissu aliyepata nafasi ya kuzungumza leo Jumatano Januari 22, 2025 baada ya matokeo kutangazwa, amesema Mbowe amewezesha kufanyika kitu kikubwa ambacho hakijawahi kufanyika tangu kuanzishwa kwa chama hicho.

“Tumefanya uchaguzi ambao hatujawahi kuufanya katika historia yetu kama chama. Tumeweka viwango vya juu kwa vyama vingine. Sasa chama chochote kama kinatuweza wafikie hicho kiwango, tumefanya uchaguzi wa kihistoria, huru na haukuwa na mizengwe.”

“Mivutano ilikuwepo, lakini hakukuwa na mizengwe, ulikuwa uchaguzi huru, kila mwenye haki ya kupiga kura alipiga kura na ilihesabiwa na kuhesabika. Matokeo ambayo tumepata yametokana na kura halali,” amesema Lissu.


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!