MATOKEO Simba SC vs CS Constantine 19 January 2025

MATOKEO Simba SC vs CS Constantine 19 January 2025
MATOKEO Simba SC vs CS Constantine 19 January 2025
Klabu ya Simba imekamilisha mpango wake wa kumaliza nafasi ya kwanza hatua ya makundi kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup) baada ya Kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya CS Constantine katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar Es Salaam.

MATOKEO Simba SC vs CS Constantine 19 January 2025
Mabao ya kipindi cha pili yaliyofungwa na Kibu Denis dakika ya 61 na Lionel Ateba dakika ya 79 yalitosha kuihakikishia Simba ushindi ambao unawafanya waongoze kundi A baada ya kufikisha pointi 13 na kuizidi CS Constantine iliyoshuka nafasi ya pili Kwa pointi 12.
Ushindi huo unamaanisha Simba itacheza mechi ya kwanza ugenini katika hatua ya robo fainali dhidi ya timu itakayomaliza nafasi ya pili katika Kundi B, C au D.