MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili UTUMISHI 27 November 2024

Filed in Usaili by on 27/11/2024 0 Comments

MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili UTUMISHI 27 November 2024MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili UTUMISHI 27 November 2024

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI),, Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Shirika la Nyumbu (TATC), Chuo cha
Diplomasia (CFR),, Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Tume ya Nguvu za AtomuTanzania (TAEC), Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE), Chuo Kikuu cha
Ushirika Moshi (MoCU) anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 03-12-2024 hadi 10-12-2024 hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

  • Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
  • Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)
  • Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
  • Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga
    kura,Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji unachotoka.
  • Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI,
    Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za
    Mwombaji.
  • Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza
    matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA
    HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
  • Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
  • Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
  • Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na
    Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
  • Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
  • Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
  • Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa iku ya usaili.

BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA MAJINA


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!