MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili MJNUAT
MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili MJNUAT
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 14-12-2024 hadi 16-12-2024 hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili
wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
- Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
- Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)
- Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
- Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga
kura,Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji unachotoka. - Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI,
Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za
Mwombaji. - Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza
matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA
HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI. - Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
- Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
- Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na
Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NEECTA) - Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi
vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika. - Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
- Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa iku ya usaili.
