MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI CHUO KIKUU CHA MJNUAT

Filed in Usaili by on 07/09/2024 0 Comments
MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI CHUO KIKUU CHA  MJNUAT

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa 

kuendeshwa kuanzia tarehe 14-09-2024 hadi 18-09-2024 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo 
yafuatayo:-
  • Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
  • Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
  • Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura,Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.
  • Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI,BStashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
  • Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
  • Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
  • Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
  • Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
  • Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
  • Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
  • Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.
Bonyeza hapa chini Kudownload PDF ya Majina.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!