MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Ajira za INEC Chunya District Council

Filed in Usaili by on 12/12/2024

MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Ajira za INEC Chunya District CouncilMAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Ajira za INEC Chunya District Council

Ofisi ya Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Uchaguzi la Lupa (Chunya) inapenda kuwataarifu wananchi walioomba kazi ya Uandishi Msaidizi pamoja na kazi Uendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki, kuwa usaili wa kazi hizo unatajarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 11 Desemba, 2024 hadi tarehe 12 Desemba, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondari Lupa na Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya (Sapanjo) uliopo karibu na Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Chunya.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Muda ni kuanzia saa 2:00 asubuhi.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

  • Usaili utafanyika kwa siku tajwa katika eneo tajwa. Aidha, kila Msailiwa azingatie tarehe na siku iliyotajwa kwenye orodha ya wasailiwa walioitwa kwenye Usaili- orodha imeambatishwa pamoja na Tangazo hili, Pia Orodha ya waombaji kwa kila kata zimebandikwa kwenye kata husika
  • Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na: – Kitambulisho cha NIDA, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha Mkazi, Hati ya Kusafiria, Leseni ya udereva, au Barua ya utambulisho kutoka ofisi ya Mtendaji wa Mtaa, Cheti chenye picha na
  • Kila Msailiwa atajigharamia Chakula, Usafiri na Malazi.

Aidha, waombaji kazi ya Uandikishaji Msaidizi pamoja na Uendeshaji wa Vifaa vya Kibayometriki ambao majina yao hayajaonekana katika Tangazo hili, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi za aina hii na kazi nyingine zitakapotangazwa na kuzingatia masharti ya Tangazo husika.

Orodha ya wanaoitwa kwenye usaili imeambatanishwa kwenye PDF hapa chini;


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Comments are closed.

error: Content is protected !!