MAJINA ya Walioitwa Kazini Bunge la Tanzania

Filed in Kuitwa Kazini by on 05/09/2024 0 Comments

MAJINA ya Walioitwa Kazini Bunge la Tanzania

Katibu wa Bunge anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali katika Utumishi wa Bunge waliotajwa katika Tangazo hili kwamba, walifaulu kushinda waombaji kazi wenzao kwenye usaili uliofanyika tarehe 24 – 29 Agosti, 2024 katika Ofisi za Bunge Dodoma.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Hivyo, wahusika wanaarifiwa kwamba wanatakiwa kuripoti kazini Ofisi ya Bunge Dodoma ifikapo tarehe 09 Septemba, 2024 kwa ajili ya kukamilisha taratibu za ajira zao na kupangiwa kazi.

Waombaji kazi wanaoitwa kuripoti kazini wanatakiwa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

  • Kufika na vyeti halisi vya masomo kuanzia Kidato cha IV na kuendelea kulingana na sifa za kazi,
  • Kufika na Cheti cha Kuzaliwa;
  • Kufika na Kitambulisho cha Taifa;
  • Kufika na Cheti halisi cha Ndoa (kama ipo); na
  • Kufika na Vyeti halisi vya kuzaliwa mtoto/watoto (kama wapo).

Kwa ambao masharti ya kazi zao yanawataka kusajiliwa na Mabaraza au Bodi zao za Kitaaluma wanatakiwa kuja na vyeti vyao vya usajili pamoja na leseni halali (valid licence) za kufanyia kazi.

TANGAZO LA KUITWA KAZINI BUNGE LA TANZANIA 04-09-2024


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!