Majeruhi Waliopokelewa Muhimbili Kutoka Kariakoo
ORODHA YA MAJERUHI WALIOPOKELEWA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI KUTOKA KARIAKOO LEO TAREHE 16.11.2024 KUANZIA SAA 04:00 ASUBUHI HADI SAA 11:00 JIONI DAR ES SALAAM: NOVEMBA 16, 2024.
Hospitali ya Taifa Muhimbili imepokea jumla ya majeruhi 40 waliopata ajali kutokana na kuporomoka kwa ghorora Kariakoo, Jijini Dar es Salaam ambapo hadi kufikia saa 11 jioni, 35 kati yao wameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kufanyiwa uchunguzi na kubainika kuwa walipata majeraha sehemu mbalimbali za mwili na kutibiwa, kisha kuruhusiwa.
Watano kati yao bado wanaendelea na matibabu ambapo wanne wamepelekwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwaajili matibabu zaidi.
Aidha Hospitali hiyo imesema kuwa haijapokea maiti.
Ifuatayo kwenye PDF hapa chini ni orodha ya majeruhi waliopokelewa Hospitali ya Taifa Muhimbili;
