MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumatatu 25 November 2024
MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumatatu 25 November 2024
Mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Tabora United dhidi ya Singida Black Stars uliokuwa uchezwe jana Novemba 24 kwenye Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Tabora umeahirishwa baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha uwanja kujaa maji.
Kutokana na kadhia hiyo, mchezo huo umepagwa kuchezwa leo Jumatatu Novemba 25, 2024 saa 4:00 asubuhi.
Akithibitisha kuahirishwa kwa mchezo huo kamishna kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Said Mkai amesema wamefanya jitihada za kuhakikisha mchezo huo unachezwa lakini imeshindikana.
Mkai amesema makubaliano ya mchezo huo kuahirishwa yamefikia kwa timu zote mbili kushirikishwa na kuamua uahirishwe.
