MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumatatu 20 January 2025
MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumatatu 20 January 2025
Mtandao wa TikTok umeacha kufanya kazi nchini Marekani, saa chache kabla ya sheria mpya inayopiga marufuku mtandao huo kuanza kutekelezwa.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Uingereza (BBC), mtandao huo umepigwa marufuku kutokana na wasiwasi kuhusu uhusiano wake na Serikali ya China na ilipewa tarehe ya mwisho ya January 19, 2025.
Rais, Joe Biden amesema kuwa ataliacha suala hilo kwa mrithi wake, Donald Trump ambaye naye pia amesema kuwa huenda atatoa msamaha wa siku 90 kwa TikTok atakapoingia madarakani kesho Jumatatu.
“Kuongezwa siku 90 ni jambo ambalo huenda likafanyika, kwa sababu ni sahihi. Ikiwa nitaamua kufanya hivyo, labda nitatangaza Jumatatu,” Trump aliambia NBC News jana Jumamosi.
Hata hivyo watumiaji waliripoti kuwa programu hiyo pia imeondolewa kwenye programu za Apple na Google za Marekani hivyo TikTok.com haikuonyesha video.
