MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumatatu 18 November 2024
MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumatatu 18 November 2024
Fadlu hii Sasa imekaa poa, Miwili wa King Kikii Kuzikwa Leo Dar, Taifa Stars vs Guinea kesho saa 10:00 jioni Kwa Mkapa, Kazi mnayo Ramovic aanza Mambo, Kiungo Spurs amtaja Diarra.
Rais Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuongoza timu ya ukaguzi wa majengo kukagua eneo lote la Kariakoo mkoani Dar es Salaam na kutoa taarifa kamili ya hali ya majengo katika eneo hilo mara baada ya zoezi la uokoaji kufuatia ajali ya jengo kuporomoka kukamilika.
Aidha, Rais Samia ameliagiza Jeshi la Polisi kupata taarifa kamili kutoka kwa mmiliki wa jengo lililoporomoka kuhusu namna ujenzi ulivyokuwa ukifanyika.
Rais Dkt. Samia ametoa maagizo hayo leo Novemba 18 akiwa nchini Brazil, alipokuwa akitoa salamu za pole kwa wananchi kufuatia tukio hilo.
Rais Samia ametoa pole kwa wafiwa na ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na tukio la kuporomoka kwa jengo hilo, na amewahakikishia wananchi kwamba kutakuwa na uwajibikaji.
