MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumatatu 13 January 2025
MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumatatu 13 January 2025

MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumatatu 13 January 2025
Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina moja la Lino, anadaiwa kuchoma moto nyumba aliyopanga mpenzi wake, Ajentina Ngimbudzi (31) katika Mtaa wa Idundilanga, Halmashauri ya Mji wa Njombe.
Akizungumza na Jumapili January 12, 2025, Ngimbudzi amedai ugomvi huo ulizuka jana saa 4 usiku baada ya Lino kufika kwenye biashara yake ya kuuza nyama na kumkuta huyo mwanaume amekaa jikoni.
“Mteja alikuwa amekaa jikoni, alipofika akauliza kwa nini yupo hapo. Nilimweleza kuwa ni mteja tu kama wateja wengine, lakini akaanza ugomvi. Mteja alikimbia, baada ya hapo Lino alikwenda nyumbani kwangu na kuwasha moto ulioteketeza baadhi ya nguo zangu na kusababisha nyumba kushika moto,” amedai Ngimbudzi.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga akizungumza kwa simu kuhusiana na tukio hilo amesema linahusishwa na wivu wa mapenzi.
