MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumatatu 02 December 2024

Filed in Magazeti by on 02/12/2024

MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumatatu 02 December 2024

Waziri wa Afya, Jenista Mhagama amesema Serikali inatumia Sh400,000 kwa Mtanzania mwenye maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) kila mwaka, sawa na Sh750 bilioni kwa Waviu milioni 1.7.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Jenista amesema hayo Jumapili ya Desemba Mosi, 2024 kwenye maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani ambayo kitaifa yanaadhimishwa mjini Songea mkoani Ruvuma, katika viwanja vya Maji Maji huku Makamu wa Rais, Dk Isdory Mpango ndiye mgeni rasmi.

“Inakadiriwa kila mwaka kila mtu anayeishi na VVU katika Taifa letu anatumia fedha zisizopungua Sh400,000 na kama tunavyojua wenye maambukizi ni milioni 1.7 nchini, hivyo tukitumia zaidi ya Sh750 bilioni kila mwaka kuhakikisha tunafubaza VVU na Ukimwi ndani ya Taifa letu.

“Gharama ni kubwa, tuna kila sababu kuzuia maambukizi mapya nchini na kuhakikisha walio katika dawa wanafubaza virusi vya Ukimwi kwa kutoa tiba stahiki na kuhakikisha Waviu wote wanaendelea kufubaza VVU na wataendelea kulindwa katika uhai wao,” amesema Waziri Jenista.


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Comments are closed.

error: Content is protected !!