MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumatano 22 January 2025
MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumatano 22 January 2025
Rais wa Marekani, Donald Trump, amesaini amri kadhaa za kiutendaji baada ya kuapishwa, ikiwemo kufuta haki ya uraia wa kuzaliwa kwa watoto wa wahamiaji haramu na wenye viza za muda.
Uamuzi huu umebadilisha tafsiri ya muda mrefu ya marekebisho ya 14 ya Katiba ya Marekani, ambayo yalikuwa yakitoa uraia wa kuzaliwa kwa yeyote aliyezaliwa nchini Marekani, bila kujali hali ya kisheria ya wazazi wake.
Kwa mujibu wa amri hiyo mpya, watoto waliozaliwa Marekani hawatatambuliwa kama raia wa nchi hiyo iwapo wazazi wao ni wahamiaji wasio halali au wana viza za muda.
Hatua hiyo itaanza kutekelezwa siku 30 kutoka sasa, na watoto watakaozaliwa nchini humo watahitajika kuwa na angalau mzazi mmoja ambaye ni raia wa Marekani au mkazi wa kudumu mwenye kadi ya kijani.
Marekebisho ya 14 ya Katiba ya Marekani, yaliyopitishwa zaidi ya karne moja iliyopita, yamekuwa msingi wa uamuzi wa Mahakama ya Juu yanayowalinda watoto wa wazazi wa kigeni waliozaliwa nchini Marekani.
