MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumapili tarehe 15 December 2024
MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumapili tarehe 15 December 2024
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, amesema Dira mpya ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 itazingatia misingi sita muhimu: Umoja, Utu, Uhuru na haki, Demokrasia, ulinzi wa maliasili na rasilimali pamoja na utamaduni na maadili ya taifa.
Akizungumza leo Jumamosi Desemba 14, 2024, wakati wa mkutano wa vyama vya siasa na Tume ya Mipango kuhusu uhakiki wa rasimu ya Dira hiyo, Profesa Mkumbo amesema mkutano huo ni sehemu ya kuhakikisha maoni ya wadau mbalimbali yanazingatiwa.
Amesisitiza kuwa Dira 2050 inalenga kuimarisha demokrasia kwa kujengwa kwa katiba imara, taasisi madhubuti za umma na mfumo wa kisiasa unaojali mwafaka wa kitaifa.
Akitaja mchango wa vyama vya siasa, amesema vimekuwa wadau muhimu wa maendeleo, na vimependekeza mambo kama matumizi ya teknolojia, ulinzi wa rasilimali, ugatuzi wa madaraka, na uwezeshaji wa vijana viwe sehemu ya Dira 2050.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Tags: MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumapili tarehe 15 December 2024