MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumapili 24 November 2024
MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumapili 24 November 2024
RAIS Samia atoa Kibali Cha Ajira za Walimu 4000, Simba Kuna jambo, Shomari Kapombe afichua Siri, Mechi nne za maamuzi Yanga, Fadlu aipigia hesabu Bravos, Wachezaji Yanga Wala kiapo kuiua Al Hilal.
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabuni amewataka viongozi wa dini ya Kikristo nchini, kuungana na kuanzisha programu maalumu ya mitaalaa ya elimu ya mafundisho ya Biblia kuanzia elimu ya awali, msingi na sekondari kwa lengo la kulinda maadili kwa vijana.
Amesema kuanzishwa kwa masomo hayo kuende sambamba na kutenga fedha kwa ajili ya uchapaji na ugawaji wa Biblia bure, zenye mtaalaa mmoja wa kufundisha baina ya dhehebu moja na jingine na kutoa ajira kwa walimu wa dini nchini.
Profesa Kabudi ametoa wito huo Jumamosi, Novemba 23, 2024 alipokuwa mgeni rasmi wakati wa ibada ya kumweka wakfu Askofu mteule wa Kanisa Baptisi Kanda ya Kusini Magharibi, Mchungaji Sylvester Mbwaga.
“Nasema hivyo kwa sababu dunia imebadilika kutokana na kukua kwa teknolojia za utandawazi, hali inayosababisha watu kufika mbali kwa kuamini Mungu hayupo jambo ambalo sio sahihi,” amesema.
Profesa Kabudi amesema lengo la kusisitiza uanzishwaji wa mitalaa ya elimu ya Biblia shuleni ni kuokoa vijana kuporomoka kimaadili na kuingia kwenye upepo mbaya.
