MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumapili 19 January 2025
MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumapili 19 January 2025
Baada ya kushindwa kutinga robo Fainali, Klabu Young Africans imekosa kiasi cha Dola 900,000 (Sh2.3 bilioni) ambacho kila timu inayotinga hatua hiyo inajihakikishia kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Yanga imeshindwa kufuzu hatua hiyo msimu huu baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 na MC Alger kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Aidha, kwa kuishia hatua ya makundi, itaondoka na kifuta jasho cha Dola 700,000 (Sh1.8 bilioni) kutoka CAF.
Msimu uliopita, Yanga iliishia hatua ya robo Fainali ambapo ilitolewa kwa mikwaju ya penalti 3-2 na Mamelodi Sundowns baada ya mechi mbili baina yao kumalizika kwa sare ya 0-0.
