MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumapili 12 January 2025
MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumapili 12 January 2025
Kaimu Mganga mkuu wa Mkoa wa Njombe Dk David Ntahindwa amesema mwaka 2024 huduma ya uzazi wa mpango ilitolewa kwa vijana balehe wapatao 35,223 (wenye umri kati ya miaka 10 hadi 24) huku zaidi ya 1,600 wakitibiwa magonjwa ya ngono.
Takwimu hizo zimetolewa Januari 11, 2025 wakati wa mkutano wa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga na waandishi wa habari mkoani hapo.
“Vijana 2,677 wenye umri kati ya miaka 10 hadi 19 walipata huduma ya matunzo na vijana balehe 1,675 walipatiwa matibabu ya magonjwa ya ngono” amesema Ntahindwa wakati akizungumza katika mkutano huo.
Katika hatua nyingine, Nderiananga amesema juhudi zinapaswa kuchukuliwa ili kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi hasa kwa kundi la vijana huko mkoani Njombe.
Amesema pamoja na jitihada za Serikali katika kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi wenyewe, bado kuna maambukizi mapya hasa kwa kundi la vijana.
