MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumanne tarehe 10 December 2024
MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumanne tarehe 10 December 2024
“Ni siku ya furaha kwangu,” ni kauli ya Hadija Shaban mama wa pacha wawili walioungana baada ya kurejea nchini kutoka Saudi Arabia akiwa na watoto wake waliopata tiba ya kutenganishwa.
Watoto hao Hussein na Hassan walipelekwa Saudi Arabia, Agosti mwaka jana na kufanyiwa upasuaji Oktoba, 2023 wa kutenganisha maeneo ya tumbo, kibofu, nyonga, utumbo mkubwa, mishipa ya damu na fahamu maeneo ambayo viliungana.
Matibabu ya kuwatenganisha Hussein na Hassan yalifadhiliwa na Serikali ya Saudi Arabia, ambayo iliahidi kufanya hivyo mwaka jana kwa watoto hao wenyeji wa Mkoa wa Tabora.
Baada ya kuwasili leo Jumatatu Desemba 9, 2024 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Hadija amesema ni furaha kwake kuwaona wapendwa wake wakiwa hai, akiishukuru Serikali kwa msaada wa kurejesha tumaini la kuwapakata watoto wake.

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Tags: MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumanne tarehe 10 December 2024