MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumanne 26 November 2024
MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumanne 26 November 2024
Klabu ya Singida Black Stars imewasimamisha makocha wake wawili, Patrick Aussems na msaidizi wake Dennis Kitambi kutokana na matokeo mabaya, huku ikidaiwa kumwania Miguel Gamondi aliyeachana na Yanga hivi karibuni.
Leo asubuhi Singida ilitoka sare ya mabao 2-2 na Tabora United kwenye Uwanja wa Al Hassan Mwinyi, mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao ulitarajiwa kupigwa jana lakini ukasogezwa mbele kutokana na uwanja kujaa maji.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo, imesema kuwa imewasimamisha makocha hao kutokana na matokeo mabaya ya timu hiyo, ambayo imepoteza mchezo mmoja na kutoka sare miwili kati mechi 11 iliyocheza chini ya makocha hao.
Hata hivyo, wakati Aussems na msaidizi wake wakiwekwa kando kuna taarifa kuwa aliyekuwa kocha wa Yanga Miguel Gamondi, amekuwa akitajwa kuwa anaweza kwenda kurithi mikoba ya Mfaransa huyo.
