MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumanne 21 January 2025
MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumanne 21 January 2025
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma ya kusambaza video za utupu maarufu ‘connection’ zinazodaiwa kuwa za wanafunzi wa Shule ya Sekondari Baobab.
Hayo yamesemwa Jumatatu ya January 20, 2025 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salim Morcase, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, huku akisema kuwa wengine zaidi wanafuatiliwa.
Kamanda Morcase amesema mtu huyo alikutwa akiwa na picha hizo kwenye kifaa cha kielektroniki kinachodaiwa kutumika kusambazia picha hizo mtandaoni.
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni wiki kadhaa tangu video za utupu zinazodaiwa kuwa ni za wanafunzi wa shule hiyo zisambae katika mitandao ya kijamii.
Mwenyekiti wa shule hiyo, Fredy Ntevi amesema shule yao inatoa elimu bora na malezi mema kwa wanafunzi, na kwamba kitendo cha kusambaza picha hizo na kuhusianisha na shule hiyo kinalenga kuichafua taasisi hiyo jambo ambalo halikubariki.
