MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumanne 19 November 2024
MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumanne 19 November 2024
Benchi la Kazi Yanga, Yanga Kupitisha Panga jingine, Stars vs Guarassy, Tanzania vs Guinea saa 1:00 Usiku Kwa Mkapa, Mbowe kuzima mnyukamo Chadema? tutawakumbuka ajali ya Ghorofa Kariakoo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameliagiza Jeshi la Polisi kuhakikisha linamtafuta popote alipo mmiliki wa jengo la ghorofa lililoporomoka jijini Dar es Salaam na kusababisha vifo vya watu 15 na kujeruhi wengine zaidi ya 80.
Pia, amesema kuwa Serikali imeunda timu ya watu 19 kwa ajili ya kukagua ubora wa majengo yote yaliyopo eneo la Karakoo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan.
Majaliwa ameyasema hayo leo Novemba 18, 2024 wakati akiongoza waombolezaji kuaga miili ya watu waliofariki baada ya kudondokewa na jengo hilo kwenye tukio lililofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
