MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumanne 14 January 2025
MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumanne 14 January 2025
Nyota wa zamani wa Taifa Stars, Mrisho Ngasa, ataungana na magwiji wengine wawili katika droo ya Fainali za CHAN2024 itakayofanyika nchini Kenya Jumatano ya Januari 15.
Wachezaji hao wa zamani wa soka ni Hassan Wasswa kutoka Uganda na Mkenya McDonald Mariga ambao wataungana na Mrisho Ngasa kutoka Tanzania.
Droo hiyo itafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta, Nairobi Kenya, Jumatano saa 2:00 usiku.
Michuano ya CHAN 2024 itaanza tarehe 1 February hadi tarehe 28 February, 2025, katika mataifa ya Kenya, Uganda na Tanzania.
