MAGAZETI ya Tanzania Leo Ijumaa tarehe 13 December 2024

Filed in Magazeti by on 12/12/2024

MAGAZETI ya Tanzania Leo Ijumaa tarehe 13 December 2024

Ni muda wa kushinda Mamilioni Kwa Kujiunga na 1Win Bofya HAPA Kujisajili, hakikisha umeweka Promo Code ambayo ni A19B ili kupata bonus ya Kujisajili.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya uwepo wa kimbunga Chido katika Bahari ya Hindi kaskazini mwa Kisiwa cha Madagascar.

Taarifa ya TMA ya leo Desemba 12, 2024 iliyopo kwenye tovuti yake imesema mifumo ya hali ya hewa inaonyesha kimbunga hicho kinatarajiwa kuelekea maeneo ya kaskazini mwa Msumbiji katika kipindi cha siku nne zijazo (Desemba 13 hadi 16, 2024).

TMA imesema kwa sasa kimbunga hicho hakiashirii uwezekano wa kusababisha athari za moja kwa moja Tanzania.

Hata hivyo, TMA imesema kutokana na ukaribu wa maeneo ambayo kimbunga Chido kinatarajiwa kupita (kaskazini mwa Msumbiji) na maeneo ya kusini mwa Tanzania, upo uwezekano mdogo wa matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa itakayoambatana na upepo mkali na mawimbi makubwa ya bahari kwa maeneo ya Mtwara na maeneo jirani hususan kati ya Desemba 14 na 16.

“Watumiaji wa bahari na wananchi kwa ujumla wanashauriwa kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalamu wa kisekta,” imeshauri TMA.


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Comments are closed.

error: Content is protected !!