MAGAZETI ya Tanzania Leo Ijumaa 29 November 2024
MAGAZETI ya Tanzania Leo Ijumaa 29 November 2024
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tamisemi, Mohamed Mchengerwa amesema katika nafasi ya uenyekiti wa kijiji Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeongoza kwa asilimia 99.01 kikifuatiwa na Chadema.
Mchengerwa ameyasema hayo leo Alhamisi Novemba 28, 2024 akitangaza matokeo ya uchaguzi huo mbele ya waandishi wa habari.
“Kwa nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji ni 12,271 kati ya nafasi 12,280 zilizopaswa kufanya uchaguzi. Kati ya nafasi hizo, CCM imeshinda nafasi 12,150 sawa na asilimia 99.01, Chadema imeshinda nafasi 97 sawa na asilimia 0.79, ACT Wazalendo imeshinda nafasi 11 sawa na asilimia 0.09, CUF imeshinda nafasi 10 sawa na asilimia 0.08.
“NCCR Mageuzi imeshinda nafasi 1 sawa na asilimia 0.01, UMD imeshinda nafasi 1 sawa na asilimia 0.01 na ADC imeshinda nafasi 1 sawa na asilimia 0.01,”amesema na kuongeza.
