MAGAZETI ya Tanzania Leo Ijumaa 24 January 2025
MAGAZETI ya Tanzania Leo Ijumaa 24 January 2025
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema maeneo yanayopata mvua za chini ya wastani hadi juu ya wastani yanatarajiwa kuwa na matukio ya hali mbaya ya hewa, kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
MATOKEO Kidato Cha Nne 2024
TMA imesema vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa kujitokeza na kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi, yanayoweza kusababisha uharibifu wa miundombinu, mazingira, mlipuko wa magonjwa pamoja na upotevu wa mali na maisha.
Maeneo yanayotarajiwa kunyesha mvua za chini ya wastani hadi wastani ni mikoa ya Pwani, Kigoma, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Morogoro, Tanga, Dar es Salaam na visiwa vya Unguja na Pemba.
Mikoa inayopata mvua za wastani hadi juu ya wastani ni mashariki mwa mikoa ya Simiyu na Mara.
Hata hivyo, Mwananchi imemtafuta Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali, Hosea Ndagala kujua walivyojipanga iwapo hali hiyo itajitokeza.
