MAGAZETI ya Tanzania Leo Ijumaa 17 January 2025
MAGAZETI ya Tanzania Leo Ijumaa 17 January 2025
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limemteua mwamuzi Ahmed Arajiga na wenzake watatu kuchezesha mechi ya Kundi B Kombe la Shirikisho Afrika kati ya RS Berkane ya Morocco na Stellenbosch ya Afrika Kusini itakayopigwa Jumapili ya Januari 19.
Timu zote mbili tayari zimefuzu hatua ya robo Fainali, Berkane ikiwa kinara wa kundi hilo baada ya kukusanya pointi 13, Stellenbosch nafasi ya pili na pointi tisa, Stade Malien nafasi ya tatu na pointi nne na Lunda Sul ikimaliza mkiani na alama mbili.
Arajiga mara ya mwisho kuchezesha mechi za CAF ilikuwa Septemba 14 mwaka jana kati ya Red Arrows na TP Mazembe kwenye hatua za pili za Ligi ya Mabingwa.
Kwenye mchezo huo, Arajiga atasaidiana na waamuzi wengine wa Tanzania Mohamed Mkono, Kassim Mpanga na Nasir Salum.
