MAGAZETI ya Tanzania Leo Alhamisi 28 November 2024

Filed in Magazeti by on 27/11/2024 0 Comments

MAGAZETI ya Tanzania Leo Alhamisi 28 November 2024

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson, amesema kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Dk Faustine Ndugulile, kimeacha simanzi kubwa kwa Bunge na Watanzania kwa ujumla, kutokana na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Taifa.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Akizungumza baada ya kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa, Mtaa wa Uzunguni A, Jijini Mbeya leo Novemba 27, 2024, Dk Tulia amesema kuwa nyota ya Dk Ndugulile imezimika wakati akiwa ameanza kung’ara katika anga za kimataifa. Alikuwa aanze rasmi majukumu yake mapya ya kimataifa Machi mwaka 2025.

Dk Tulia amesema kuwa Bunge limepoteza mbunge mahiri ambaye pia alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi. Mchango wake uliwezesha kufanikisha mabadiliko makubwa ya sheria na sera katika sekta za afya na mapambano dhidi ya Ukimwi.

Aidha, amewataka Wananchi wa Kigamboni kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho wamempoteza mbunge wao na kumuombea apumzike kwa amani.

Dk Ndugulile amefariki dunia usiku wa kuamkia leo India alipokuwa akipatiwa matibabu.


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!