MAGAZETI ya Tanzania Leo Alhamisi 23 January 2025

Filed in Magazeti by on 22/01/2025 0 Comments

MAGAZETI ya Tanzania Leo Alhamisi 23 January 2025

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amesema Jeshi la Polisi litaendelea kutekeleza jukumu lake la kikatiba kwa kusimamia usalama katika mikutano na shughuli za vyama vya siasa bila kujali itikadi ya chama chochote.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Bashungwa amelipongeza jeshi hilo kwa kusimamia ulinzi na usalama kwa weledi katika mkutano mkuu wa CCM uliofanyika Dodoma pamoja na wa Chadema uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Bashungwa amesema hayo leo Januari 22, 2025 wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dodoma na kusisitiza kuwa, vyama vya siasa kutimiza wajibu wa kutii sheria bila shuruti ili kuepuka kulazimishwa kutii sheria.

“Matarajio yangu ni kwamba haki hii mnayoitenda Jeshi la Polisi kwa kutoangalia itikadi, pia vyama vya siasa kwa jumla, haki hii ije na wajibu kwa wao kutii sheria bila shuruti, hakuna haki bila wajibu” amesisitiza Bashungwa.

Ameliagiza Jeshi la Polisi kuendelea kujipanga kusimamia kikamilifu usalama kwa raia na mali zao wakati wa uchaguzi madiwani, wabunge na Rais utakaofanyika mwaka huu 2025 ili kuendelea kudumisha usalama, amani na utulivu wa nchi yetu.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Camillus Wambura ameeleza kuwa Jeshi la Polisi limejiimarisha vyema kwa kuweka mikakati dhabiti ya kuimarisha usalama kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka huu.


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!