MAGAZETI ya Tanzania Leo Alhamisi 21 November 2024

Filed in Magazeti by on 21/11/2024 0 Comments

MAGAZETI ya Tanzania Leo Alhamisi 21 November 2024

Mashine ya Kwanza yatua Yanga, Dube, Mzize Kazi ipo, Fadlu ateta Kuhusu Manula na Camara, kesho Ijumaa Pamba Jiji vs Simba SC saa 10:00 jioni, Rekodi za Msuva zilivyoibeba Taifa Stars AFCON, Kivumbi Kampeni Uchaguzi Serikali za Mitaa Zikianza, Rais Samia hatutajuta kubomoa Majengo.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Ombi la Jackson Clement, mwanafunzi wa kidato cha nne aliyenusurika kifo kwenye ajali ya ghorofa Kariakoo, limesikika baada ya Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) kumhakikishia hatapoteza haki yake.

Clement ni miongoni mwa manusura wa ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa nne, Kariakoo jijini Dar es Salaam, lililosababisha vifo vya watu 16 na majeruhi zaidi ya 86 na uharibifu mali za mamilioni ya shilingi November 16, 2024.

Jana Jumanne, Novemba 19, 2024, Clement ambaye ni mwanafunzi wa sekondari ya Charambe, alisimulia kisa chake kuwa huwa anakwenda kumsaidia shemeji yake siku za mwisho wa wiki, na kuwa siku anakutwa na mkasa huo alikwishafanya mitihani saba ya kuhitimu kidato cha nne.

Mitihani ya kidato cha nne, ilianza November 11 na itamazika November 29, 2024.

Jumatano November 20, 2024, Gazeti la Mwananchi limemtafuta Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Said Ally Mohamed kufahamu hatima ya maombi ya Clement, na kuwajibiwa kuwa mwanafunzi huyo hatapoteza haki yake ya kumaliza mtihani wake wa mwisho.

Dk Mohamed amesema baraza litatumia kanuni zake katika kushughulikia suala hilo na mwanafunzi huyo hatapoteza haki yake ya mtihani.


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!