MAGAZETI ya Tanzania Leo Alhamisi 05 December 2024

Filed in Magazeti by on 05/12/2024

MAGAZETI ya Tanzania Leo Alhamisi 05 December 2024

Chama cha ACT- Wazalendo kimedai madaktari wanaomhudumia Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa chama hicho, Abdul Nondo katika Hospitali ya Aga Khan wamebaini mwili wa kijana huyo kuwa na kiwango kikubwa cha sumu.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Hadi sasa kwa mujibu wa chama hicho, wataalamu hawajafahamu kama sumu hiyo imetokana na athari za kupigwa na kuteswa au alipewa kitu chenye sumu na watekaji wake.

Nondo anapatiwa matibabu Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam, baada ya kutekwa na watu wasiofahamika alfajiri ya Desemba 1, 2024 stendi ya mabasi ya Magufuli, Mbezi jijini humo mara baada ya kuwasili akitokea Kigoma kwenye shughuli za kisiasa.

Baada ya tukio hilo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime alisema kuna mtu mmoja mwanaume amekamatwa kwa nguvu na kuchukuliwa na watu waliokuwa wakitumia gari nyeupe lenye usajili wa namba T 249 CMV Land Cruiser. Huku akisema wanaendelea na uchunguzi kubaini waliohusika.

Leo Jumatano (Jana), Desemba 4, 2024, Ngome ya vijana wa chama hicho imetoa taarifa kwa umma kuelezea mwenendo wa matibabu ya kiongozi wao. Taarifa hiyo imetolewa na Philibert Macheyeki, Katibu wa Habari na Uenezi wa ngome hiyo.


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Comments are closed.

error: Content is protected !!