LIGI Kuu ya NBC ya 4 Kwa Ubora Afrika 2024

LIGI Kuu ya NBC ya 4 Kwa Ubora Afrika 2024
LIGI Kuu ya NBC ya 4 Kwa Ubora Afrika 2024
Ligi Kuu ya Tanzania imetajwa kuwa ya nne kwa ubora Afrika na ya 57 duniani kwa mwaka 2024 ikiipiku Ligi ya Afrika Kusini na Tunisia.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS) limeitangaza Ligi Kuu ya Tanzania (NBC Premier League) kupanda nafasi mbili kutoka nafasi ya sita mwaka 2023, huku mafanikio hayo yakitajwa kutokana na juhudi za vilabu vikubwa nchini vya Simba na Yanga.
Klabu ya Simba imetengeneza historia kwa kufika hatua ya makundi ya michuano ya CAF mara sita mfululizo, wakati Yanga ikitinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu wa 2023/2024 na kucheza Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF msimu wa 2022/2023.
Ligi ya Misri yenyewe imeshika nafasi ya kwanza, Botola ya Morocco ya pili, League A ya Algeria ya tatu Ligi Kuu Tanzania Bara ya nne na Ligue Pro 1 ya Tunisia ikifunga tano bora Afrika.

LIGI Kuu ya NBC ya 4 Kwa Ubora Afrika 2024
