LAKRED Ampisha Elie Mpanzu Simba SC

Filed in Michezo by on 27/09/2024

LAKRED Ampisha Elie Mpanzu Simba SCUongozi wa Klabu ya Simba SC umemuomba golikipa Ayoub Likred, iondoe jina lake kwenye mfumo wa usajili na kuingiza jina la winga mpya Elie Mpanzu Kibisawala.

Pamoja na kuondoa jina lake kwenye mfumo Ayoub ataendelea kuwa mchezaji wa Simba na kulipwa mshahara na stahiki zingine mpaka mwisho wa msimu.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Simba wamefikia hatua hiyo kutokana na mkataba wa Ayoub kuwa na kipengele cha kulipwa dola 250,000 (Zaidi ya milioni 680 za Kitanzania) ili kuvunja mkataba wake.

Simba wamefikia maamuzi ya kutovunja mkataba wake na iwapo Ayoub atapona kabla ya dirisha dogo watamtoa kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu.

Elie Mpanzu Kibisawala raia wa DR Congo mwenye umri wa miaka 22 ataruhusiwa kucheza kombe la shirikisho Afrika 2024/2025 kuanzia hatua ya makundi huku akisubili dirisha dogo la usajili mwezi December 2024 ili kuruhusiwa kucheza Ligi Kuu ya NBC.

Baada ya usajili wa Mpanzu kuingizwa kwenye mfumo Sasa Simba itakuwa na wachezaji 12 wa Kimataifa wanaoruhusiwa kutumika kwenye Ligi Kuu ya NBC ambao ni, Jean Charles Ahoua, Valentin Nouma, Mousa Camara, Chamou Karaboue, Che Fondoh Malone, Augustine Okejepha, Debora Fernandez, Fabrice Ngoma, Joshua Mutale, Lionel Ateba, Steven Mukwala na Elie Mpanzu.


JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Comments are closed.

error: Content is protected !!